Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Hemedi Majid Mwanga ametoa agizo kwa Viongozi wa Serikali ya kijijiji Cha Nyangala Bondeni kilichopo kata ya Maguha Wilayani Kilosa kuhamasisha wananchi kuchangia michango ya ujenzi wa Zahanati kupitia kuku wanaowafuga majumbani mwao.
Ametoa agizo Hilo Juni 11 Mwaka huu 2022 katika Kijiji hicho Cha Nyangala Bondeni kilichopo kata ya Maguha katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza changamoto zinazowakabili Wananchi na kuzitatua Wilayani Kilosa.
Mkuu wa Wilaya Majid ameeleza kuwa Wananchi hao wamekuwa wakimiliki mifugo mbalimbali ikiwemo kuku mmoja kuuzwa elfu kumi, hivyo kupia kuku hao wachange Kama michango yao ili waweze kijenga Boma la Zahanati ambapo Serikali itasaidia Mabati kwaajili ya umaliziaji ,hivyo Viongozi wote wa kata na Kijiji hicho amewataka washilikiane kijenga Zahanati ambapo kauli mbiu ya Ujenzi huo ni "Jenga Zahanati kwa kuku" kwanii kuku Ana thamani kubwa .
Sambamba na Hilo Mkuu wa Wilaya Majid Mwanga amewataka Watendaji wa Vijiji na Kata hiyo kuacha kuwatoza fedha Wananchi Mara wanapokwenda kupata huduma ,watambue kuwa kwa kufanya hivyo watachukuliwa hatua Kali ambapo Viongozi hao waliweza kukili kosa Hilo mbele ya Mkutano huo ya kuwa hawatarudia kutoza fedha kwa wananchi wao..
Awali Wananchi wamelalamika kutozwa fedha na Viongozi wa Serikali za Vijiji na Kata Mara wanapokwenda kupata huduma ofisi za Vijiji na Kata .
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa