Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi ametoa wito kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kuweka mkakakati madhubuti ili kuhakikisha mapato yote ya serikali yanapatikana hasa katika kipindi hiki cha ukusanyaji mapato ili kufikia lengo la kukusanya shilingi bilioni 3.3
Mgoyi amesema hayo wakati alipokuwa akitoa nasaha katika kikao cha baraza la madiwani wilayani Kilosa na kusema kuwa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ipo tayari kusaidia katika kutimiza mkakati huo lengo ikiwa ni kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa katika kufanikisha ukusanyaji wa mapato.
Mgoyi amesema mapato kwa sasa yapo chini sana hivyo ipo haja ya kujitathmini upya kwani fedha zinatakiwa kukusanywa toka kwa wananchi na kwamba kamati ya fedha isimamie zoezi zima la ukusanyaji mapato na kuhakikisha kila mmoja anahusika kwani msimu huu ni msimu wa mavuno na kwa asilimia kubwa Kilosa inategemea kukusanya mapato yake kupitia kilimo
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Hassan Mkopi ambaye ni diwani wa kata ya Mvumi amewaagiza watendaji wa kata zote kusimamia mawakala lengo ikiwa ni kuhakikisha yanapatikana mapato stahiki kulingana na kinachopatikana na kwamba mtendaji atakayeshindwa kufanya hivyo hatua za kisheria zitachukua mkondo wake.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa