Imeelezwa kuwa ili kuwa na afya bora ni lazima kuzingatia suala la lishe bora ambapo lishe inapaswa kuzingatiwa tangu mimba inapotungwa jambo litakalosaidia mtoto kuzaliwa akiwa na afya bora sambamba na kuzingatia upatikanaji wa lishe bora jambo litakalosaidia kuwa na jamii yenye afya bora.
Hayo yamebainishwa na Katibu Tawala Wilaya Yohana Kasitila ambaye ameyasema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilayak ambapo amesema kuwa suala la lishe ni suala nyeti ambalo ni shirikishi kwa viongozi wa ngazi zote pamoja na wananchi ili kuwa na jamii yenye siha njema.
Viongozi wa Wilaya na watendaji wa kata wakisaini Mkataba wa Lishe na Chanjo
Kasitila amesema kuwa mwili wa binadamu ni kama gari ambapo muda wote mwili unapaswa kuhudumiwa kwa kuzingatia lishe endelevu ili kwani Wilaya inategemewa kuwa na jamii yenye afya njema ambapo ametaka kuungwa mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha jamii inakuwa na lishe endelevu ikiwemo kusimamia suala la chanjo ya Uviko-19, chanjo ya polio kwa watoto chini ya miaka mitano inayotarajiwa kuzinduliwa kitaifa Aprili 28, 2022 kwa maslahi ya maisha ya wananchi.
Naye Mbunge wa jimbo la Mikumi Mh. Dennis Londo amesema suala la lishe pamoja na chanjo ya Covid 19 na polio ni suala la afya kwa jamii na taifa kiujumla ambapo ili jamii iweze kufanya kazi zake lazima lishe bora izingatiwe ili jamii na taifa kiujumla liweze kuwa na watu wenye uwezo wa kufanya shughuli zake kwa ufanisi hivyo ili kupata kizazi chenye nguvu ni lazima kuwekeza kwenye lishe
Londo amesema ni vema kuwekeza katika lishe kwani chakula ni dawa ambapo jamii ikila kwa mpangilio itasaidia Serikali kuepuka gharama kubwa za kuagiza madawa badala yake fedha hiyo kutumika kwa shughuli za maendeleo huku akisisitiza umuhimu wa chanjo kwani ni kinga ambayo ikizingatiwa itasaidia kuepuka maradhi lakini pia ametaka kuzingatiwa chanjo ya polio ambayo itasaidia kukinga watoto dhidi ya udumavu na kifo endapo chanjo zote hazitazingatiwa .
Mganga Mkuu Wilaya Dkt. George Kasibante
Afisa Lishe Wilaya Bi. Zaina Kibona
Mratibu wa Chanjo Wilaya Bi,Rakhia
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa