Maafisa Maendeleo ya Jamii wilayani Kilosa wamepatiwa Mafunzo ya kutumia Mfumo wa Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) ili kuwasaidia wafanyabiashara wilayani Kilosa kujisaili katika mfumo huo kwa lengo kuwainua wananchi kiuchumi.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mei 22, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, Katibu Tawala wa Wilaya Bi. Salome Mkinga amewataka watumishi hao kutumia weledi katika kutekeleza zoezi hilo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya faida za kujisajili katika mfumo huo na kwa kiwango gani mwananchi anavyoweza kunufaika.
Pia Bi. Mkinga ameongeza kuwa Mfumo huo utaweza kutoa tathimini halisi inayoonesha wananchi wa Kilosa wanahitaji nini ili waweze kukua kiuchumi hivyo amewataka maafisa maendeleo kufanya kazi kwa ushirikiano katika kusimamia na kutekeleza zoezi hilo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Ndg. Michael J Gwimile amewata Maafisa Maendeleo Jamii kuilewa na kuwaelimisha wananchi juu ya matumizi na manufaa ya mfumo huo.
Naye Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii wilayani Kilosa Ndg. Alto Mbikiye amesema mfumo huo utaweza kuwainua wananchi kiuchumi hususani wafanyabishara awe mmoja mmoja au kikundi kwa kujisaili na kutoa taarifa zao katika mfumo huo ambapo utaweza kurahisisha kujua mahitaji ndani ya kata na wilaya kiujumla ambapo serikali itaweza kufanya tathimini na kujua namna ya kutoa msaada.
Aidha Mbikiye amesema kuwa mfumo huu utaleta muunganiko kati ya mfanyabiashara mdogo na mfanyabiashara mkubwa kwa ujumla lengo ni kuwainua wananchi kuichumi na mpango huo umejikita katika makundi makubwa matatu ambayo ni wanawake, vijana na makundi maalum .
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa