Maafisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa wamegawiwa vishikwambi kwa lengo la kuongeza ufanisi kwenye kazi zao.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Bw. Selemani Kasugulu amewataka maafisa hao kutumia vitendea kazi hivyo kwa ajili ya utoaji wa taarifa, usajili wa wafugaji na Mifugo kwenye zoezi la chanjo ya Kitaifa inayoendelea Wilayani humo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Bw. Elia Shemtoi amewataka maafisa hao kuvitunza vishikwambi hivyo.
Zoezi la ugawaji wa vishikwambi lilifanyika Wilayani Kilosa mwishoni mwa wiki
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa