Mkuu wa wilaya ya Kilosa Shaka H. Shaka amewataka maafisa Kilimo kutumia pikipiki walizopewa kwa matumizi sahihi yaliyokusudiwa kwa kuhakikisha kunakuwa na tija kwa wakulima na wilaya kiujumla kwani wilaya ya Kilosa mapato yake kwa asilimia kubwa yanatokana na kilimo.
Shaka ameyasema hayo Aprili 6 wakati wa kukabidhi pikipiki 87 kwa maafisa kilimo zilizotolewa na wizara ya kilimo ambapo amesema kuwa Serikali imetoa kipaumbele katika sekta ya kilimo kwa kuongeze bajeti ya kilimo ili kukidhi mahitaji na changamoto mbalimbali za kilimo kwani kilimo ni biashara lakini pia ni maisha na kwamba ni mategemeo ya Serikali kuona wananchi wananeemeka kupitia kilimo.
Aidha amewataka maafisa hao kutumia vyombo hivyo kwa matumizi sahihi kwa kumuunga mkono Mheshimiwa Rais katika kutimiza maono ya ajenda ya 10/30 ni kwa kutekeleza ajenda hiyo katika kuinua kilimo na kwamba Wilaya Aidha inaamini hakutakuwa na malalamiko toka kwa wananchi juu ya maafisa hao kutowatembelea kwani tayari wamewezesha usafiri wa kuwafikia wakulima na kuwa msaada kwao.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Mh.Wilfred Sumari amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia mfuko wa Serikali na kutoa pikipiki 87 kwa maafisa kilimo wa Wilala ya Kilosa ambapo ametoa rai pikipiki hizo zitumike kwa matumizi sahihi na kila mmoja atambue na kuheshimu taalama yake na kwamba Halmashauri inategemea tija kutokana na uzalishaji kuongezeka utakaotokana na maafisa hao kuwajibika ipasavyo kwani Wilaya inategemea pato lake kupitia kilimo, huku akiwataka kuwa sehemu ya kuhakikisha mapato yanayotokana na kilimo yanakusanywa ipasavyo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Bi.Fauzia Nombo amewataka maafisa hao kuzingatia uaminifu na uadilifu katika matumizi ya vyombo vya moto vinavyotolewa na Serikali, ikiwemo kufanya ukaguzi wa mara kwa mara sambamba na kutumia kwa usahihi kwani Halmashauri haitegemei Afisa yoyote kutumia kwa matumizi yasiyo sahihi lakini pia hakutakuwa na malalamiko kwani watapatikana muda wote kutokana na uwepo wa usafiri anategemea utendaji wa kazi utakuwa na tija zaidi kwani watawafikia wakulima na kutoa elimu na msaada kwa mujibu wa majukumu yao, hivyo kupelekea utendaji kazi wa kiwango cha kuridhisha.
Akizungumzia upande wa ugawaji wa pikipiki hizo Mkuu wa Divisheni ya Kilimo na Mifugo Wilaya Dkt. Yuda Mgeni amesema kufuatia upatikanaji wa pikipiki hizo umepelekea maafisa kilimo wote 102 kuwa na pikipiki jambo ambalo litasaidia kuleta mabadiliko kwa wakulima katika uzalishaji kwani watapata huduma kwa wakati,huku Mkuu wa Polisi Wilaya akitoa msisitizo katika matumizi sahihi na sio kwa matumizi binafsi kwani pikipiki hizo ni mali ya Serikali huku akiwataka kuhakikisha wanaziendesha kwa umakini ikiwemo kuvaa kofia ngumu, na kutopakia zaidi ya mtu mmoja.
Jacob Mloka na Khadija Abdala kwa niaba maafisa Kilimo wenzao wamemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwatazama kwa jicho la tatu na kuwapatia usafiri ambao utawaongezea ufanisi wa kazi kwani zitawasaidia kuwafikia wakulima kwa wakati na kuleta tija katika sekta ya kilimo kwa Wilaya ya Kilosa.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa