Wito umetolewa kwa Maafisa Ugani na Maafisa Maendeleo ya Jamii waliopatiwa mafunzo kwa vitendo ya Mfumo wa fursa na vikwazo kwa maendeleo kuendeleza yale waliyofundishwa ili Elimu waliyoipata ilete matokeo mazuri kama ilivyokusudiwa.
Wito huo umetolewa Oktoba 4, 2024,na Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Hombolo Ndg.Lubuva Elisei na kusema kuwa Wakufunzi hao ngazi ya Kata wanajukumu kubwa la kuhakikisha kuwa Mfumo wa MUKI Unafanya kazi huku akiwasisitiza kuingia na kuendelea kujifunza kupitia vitini vya mada mbalimbali zinazowekwa katika mfumo ili kuleta matokeo chanya katika jamii.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Utawala bora na Ushirikishwaji wa Wananchi kutoka PS3+ D.k.t Nazar Sola amesema kuwa walichagua Kilosa kuwa Wilaya ya mfano katika kufanya mafunzo hayo kutokana na kufanya vizuri katika mafunzo ya awali na pia kutokana kuwa na Kata nyingi, hivyo amewataka Maafisa hao kuithibitishia Serikali kuwa Mfumo huo unaweza kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.
Amewasisitiza kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia yale waliyofundishwa ili kuwasaidia Wananchi Kuibua Miradi wanayohitaji na kujiona sehemu ya miradi hiyo kutokana na ushiriki wao kuanzia hatua za awali.
Naye Mratibu wa O & OD Kutoka Wizara ya TAMISEMI Bi Stella Sasita Amesema kuwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Zoezi hilo limefanyika kama Mfano hivyo kama likifanikiwa kuzaa matunda mfumo huo utazinduliwa katika Halmashauri mbalimbali ili uweze kutumika rasmi.
Amesema kuwa kuwepo Kwa Mfumo huo wa MUKI kutarahisisha na kutatua changamoto ya kutokuwepo kwa fedha za kwa baadhi ya Halmashauri,kwa upande mwingine ameyashukuru mashirika PS3+, na JIKA kwa kufanikisha mafunzo hayo kwa awamu zote.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa