Maafisa Ugani na Maendeleo ya Jamii ngazi ya Kata Wilayani Kilosa wamepatiwa Mafunzo ya mfumo wa Fursa na vikwazo kwa vitendo lengo likiwa ni kuwawezesha kuhamasisha Wananchi kuibua Miradi ya Maendeleo kulingana na Mahitaji yao pasipo kutegemea Serikali kuu.
Akizungumza wakati wa Mafunzo hayo Oktoba 3,2024 Mratibu wa O &OD Mkoa wa Morogoro Ndg.Gibson Mwakoba amesema kuwa mafunzo hayo ya siku 2 yanatolewa kwa ushirikiano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro, Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo na Wizara ya Tamisemi kwa udhamini Shirika la Jica na PS3+.
Mwakoba amesema kuwa mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu ya pili ndani ya Wilaya ya Kilosa ambapo awali mwaka 2023, mwezi Novemba yalitolewa kwa nadharia na awamu hii yametolewa kwa vitendo lengo likiwa ni kuwajengea uwezo Wakufunzi hao ngazi ya kata kutumia mfumo huo wa ujifunzaji.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala Bora na ushirikishwaji wa Wananchi kutoka Mradi wa Uimarishaji Mifumo katika Sekta za Umma Dokta Nazar Sola amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuwajengea uwezo wawezeshaji ngazi za Kata waweze kwenda kuhamasisha Wananchi kuibua Miradi itakayokidhi matarajio yao na kujiletea maendeleo huku wakipata ufahamu wa majukumu yao katika kujiletea maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa