Mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza wilayani Kilosa Dokta Eliudi Chiduo ametoa wito kwa wananchi kujijengea tabia ya kupima afya mara kwa mara kwani inasaidia kujijua kiafya na kutambua kwa haraka magonjwa yanayokukabili ili kuchukua hatua stahiki kwa wakati muafaka ikiwemo kuunganishwa na kliniki husika kwa ajili ya huduma endelevu katika hospitali ya wilaya.
Dokta Eliud amesema hayo Mei 31, 2018 wakati wa zoezi zima la upimaji uzito, kisukari, maambukizi ya virusi vya ukimwi na uchangiaji damu kwa madiwani na wakuu wa idara wakati vikao vya baraza la madiwani vikiendelea lengo ikiwa ni kuwatumia madiwani na wakuu hao wa idara kutumika kama hamasa kwa wananchi na jamii nzima.
Eliud amesema kupitia zoezi hilo watakukusanya damu salama na kukuza benki ya damu kwa ajili ya hospitali ya wilaya lakini pia watatambua walio na uzito hatarishi na magonjwa ya kisukari, shinikizo la damu na kifua kikuu bila kujijua hivyo watawasaidia kwa kuwapa ushauri juu ya lishe na matumizi ya dawa husika kwa kushirikiana na hospitali ya St Kizito Mikumi.
Aidha Dokta Eliud amesema kwa upande wagonjwa wa kisukari na shinikizo la damu mgonjwa atakayebainika kuwa nao atapatiwa ushauri pamoja na utaratibu wa ulaji chakula pamoja na dawa hali itakayomsaidia mgonjwa kupata ushauri lakini pia kukabiliana na ugonjwa husika kwa kufuata masharti.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa