Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam khigoma Malima amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya kilosa kusimamia vyema shughuli mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo na ukusanyaji wa mapato ili kuleta maendeleo kwa wananchi kama walivyoahidiwa katika ilani ya Chama cha Mapinduzi
.
Ameyasema hayo wakati wa kikao maalumu cha Baraza la Madiwani cha kujadili hoja na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kilichofanyika mwishoni mwa juma lililopita katika Ukumbi wa Chuo cha Maendeleo FDC ambapo amesema kuwa Halmashauri hii ni ya kwao hivyo wanajukumu la kuhakikisha inafanya vizuri katika Nyanja zote.
Mh Malima amesema kuwa Madiwani wanawawakilisha wananchi ambao kimsingi ndiyo waliowapa dhamana ya kuongoza hivyo jukumu lao kubwa ni kuhakikisha Halmashauri inasimama na kuwa moja kati ya Halmashauri bora za Mkoa na Taifa kwa ujumla kwa kusimamia miradi ya maendeleleo na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kwa ubora,kukuza mapato na kuyasimamia ili yaweze kuleta tija kwa Wananchi wa wilaya hiyo.
Amesema kuwa Halmashauri ya wilaya ya kilosa ni kongwe na pia ina idadi kubwa ya watu ambao ni takribani laki 617,032 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022,hivyo iko kwenye nafasi nzuri ya kuwa na mapato makubwa ukilinganisha na Halmashauri nyingine hivyo amewasisitiza kusimamia vyema suala la kuongeza ukusanyaji wa mapato ili yaweze kuleta tija kwa wananchi.
Kwa upande mwingine amewataka wataalamu wa Halmashauri kufanya kazi kwa bidii,weledi na kuheshimiana ili kufikia malengo ya kupeleka huduma na maendeleo kwa wananchi wa Kilosa kama inavyokusudiwa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mh Dokta Samia Suluhu Hassan.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa