Wito umetolewa kwa waheshimiwa madiwani kuwa sehemu ya watoa elimu kwa wananchi katika kutunza miundombinu ya barabara katika maeneo yao kwa kuwaelimisha wananchi kutopitisha mifugo kwenye barabara zilizofanyiwa matengenezo, uendelezaji wa makazi bila kufuata sheria ya mipaka ya barabara sambamba na kutotupa taka kwenye mifereji ya maji ya mvua na kusababisha kuziba kwa makalvati.
Wito huo umetolewa na Meneja wa TARURA Wilaya Injinia Harold Sawaki wakati wa kuwasilisha bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini(TARURA) ambapo amesema mpango wa bajeti umegawanyika katika makundi manne ikiwemo matengenezo ya barabara, ukarabati wa barabara na madaraja, ukarabati wa barabara na madaraja kwa miradi ya maendeleo kwa fedha za majimbo na bajeti ya fedha za miradi ya maendeleo(fedha za tozo ya mafuta ukarabati wa barabara na madaraja) ambazo bajeti inayoombwa ni kiasi cha shilingi bilioni 45 huku akisema kuwa bajeti hiyo imezingatia kukamilisha miradi viporo, uimarishaji wa barabara zenye hali nzuri kwa kuzijengea mifereji ya maji na makalvati na vipaumbele vya matengenezo ya barabara vilivyowasisilishwa kutoka kwenye kata.
Akibainisha changamoto zinazoikabili TARURA amesema ni uchache wa watumishi, ufinyu wa bajeti inayotolewa kwa ajili ya matengenezo ya barabara, wakandarasi wazawa kuwa na mitaji midogo na kutokuwa na wataalam walioajiriwa na kampuni husika hivyo kupunguza ufanisi katika utekelezwaji wa kazi za matengenezo ya barabara na madaraja, ukosefu wa maeneo ya kuchimba madini ujenzi kama vile mawe, mchanga na kokoto na uelewa mdogo wa wananchi juu ya utunzaji wa miundombinu ya barabara.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Mh. Wilferd Sumari amewataka waheshiniwa madiwani na watendaji wa kata kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa miundombinu ya barabara kwa kuhakikisha wananchi walioko katika maeneo yao wanatunza miundombinu hiyo badala ya kuwaachia TARURA jukumu hilo peke yao huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Kisena Mabuba akisema kuwa tokea kuanzishgwa kwa TARURA kazi nyingi zimekuwa zikifanyika kwa kasi na kwamba ipo kwa mujibu wa sheria hivyo ni vema waheshimiwa madiwani wakaendelea kuwasiliana nao kwa changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa