Waheshimiwa madiwani wametakiwa kutambua kuwa ili kuwa na utawala bora wanao wajibu wa kushugulika na changamoto zinazowakabili wananchi kwa kuhakikisha vikao vya kisheria vinafanyika inavyostahiki kwani vikao hivyo ni njia mojawapo ya kushughulika na kero za wananchi lakini pia kujiletea maendeleo katika maeneo yao.
Mh. Prof Palamagamba Kabudi Mbunge wa Jimbo la Kilosa Mjini
Mh. Dennis Londo Mbunge wa Jimbo la Mikumi
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya Kilosa Adam Mgoyi wakati akitoa salam zake katika baraza la madiwani ambapo amewataka kuhakikisha wanasoma kanuni za Halmashauri na taarifa mbalimbali zinazotoka kwa wataalam lakini pia kujenga ushirikiano katika kutatua kero mbalimbali pamoja na kutekeleza maagizo yote yanayotolewa na Serikali Kuu ili halmashauri iweze kwenda vizuri.
Aidha amesema anatambua kazi kubwa iliyofanyika katika ukusanyaji wa mapato kwani kipindi cha mwaka 2016 hali ya makusanyo ya mapato ilikuwa billion 1.6 lakini kwa sasa hali ni nzuri makusanyo ni bilioni 4 hii ikiwa kazi iliyofanyika kwa ushirikiano mkubwa kutoka kwa madiwani hata hivyo vyanzo vingi vya mapato bado havijafikiwa hivyo ipo haja ya kuendelea kusimamia, kukusanya na kuvifikia vyanzo vyote vya mapato ambavyo havijafikiwa lakini pia amewataka madiwani kushirikiana na Halmashauri kuwa na mpango mkakati wa kuandaa master plan ya mji wa Kilosa kwani shughuli mbalimbali zitaongeza kupitia ujenzi wa reli ya mwendo kasi unaoendelea ambapo inategemewa kuwa na ongezeko la watu kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Asajile Mwambambale amesema kama viongozi tunao wajibu wa kuweka mazingira bora ya kujifunza kwa ajili ya kizazi chetu katika sekta ya elimu msingi, sekondari na vyuo kwa kuhakikisha kunakuwa na huduma bora na mazingira mazuri ya kujifunzia lakini pia kuhimizana katika kuwekeza katika kilimo kwani Kilosa ina ardhi nzuri kwa ajili ya kilimo.sambamba na kuchochea maendeleo huku akiwasihi madiwani hao kufanya kazi kwa kushirikiana na kwamba uwezo wa halmasha uri kujiendesha na kuhudumia wananchi wake kwasasa hali ni nzuri.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Mh. Wilfred Sumari
Pamoja na hayo baraza hilo liliambatana uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmaushari na Makamu wake ambapo Mh. Wilfred Sumari alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na Makamu akiwa ni Mh. Vicent Lusinde ambapo Mwenyekiti huyo amewataka madiwani wenzake pamoja na uongozi wa Halmashauri na Wilaya kiujumla kumpa ushirikiano wa kutosha katika kusimamia makusanyo na matumizi ya fedha kutoka Serikali Kuu na Halmashauri ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa