Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mh Shaka Hamdu Shaka amelazimika kutembea zaidi ya kilomita 5 ndani ya maji baada ya kuzungukwa na maji ikiwa ni katika harakati za kuokoa wananchi waliopatwa na kaddhia ya maji kwenye makazi yao kufuatia kujaa kwa mto Miyombo baada ya kupokea maji mengi kutoka milimani.
Awali Mkuu wa Wilaya na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama walifika eneo la daraka linalounganisha vijiji vitatu katika kata ya Zombo ambalo limechukuliwa na maji na kusababisha huduma za usafiri na usafirishaji kusimama, ambapo wakiwa katika eneo hilo maji yaliendelea kuwazingira hali iliyopelekea kutembea umbali mrefu ili kujinususru na kuwasaidia wananchi walikuwa bado wapo katika eneo hilo kama makazi yao.
Kujaa kwa maji hayo kumesababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha milimani ambapo licha ya uwepo wa kadhia hiyo hakuna athari za kibinadamu zilizojitokeza zaidi ya kuharibu miundombinu ya madaraja, barabara na makazi ya wananchi kwa kaya 120 kuingiliwa na maji.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa