Wakulima, Wafugaji na Wavuvi nchini wametakiwa kuzitumia teknolojia mpya, tafiti na takwimu sahihi zinazotolewa wakati wa Maonesho ya Nanenane nchini kuongeza tija katika uzalishaji, usindikaji, na ubora wa mazao ili kuifanya sekta ya kilimo kuchochea ajira, kukuza uchumi na kuongeza pato la wananchi na Taifa kwa ujumla.
Rai hiyo imetolewa Agosti 8, 2022 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge Mh.George Simbachawene wakati akifunga maonesho ya Wakulima(NaneNane) Kanda ya Mashariki ambapo ameagiza shughuli za zinazofanyika wakati wa maonesho hayo kuwa endelevu kwa mwaka mzima ili kufanya eneo hilo kuwa kitovu cha teknolojia katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.
Mhe. Simbachawene amesema Kanda ya Mashariki inayo fursa nyingi zikiwemo za Viwanda na Uwekezaji ambapo ametaka Wakulima, Wafugaji na Wavuvi kutambua fursa hizo lakini pia wahakikishe wanazifikisha kwa jamii ili iweze kunufaika nazo pamoja na bunifu za aina mbalimbali.
Wa kwanza kushoto Mh.George Simbachawene, wa katikati Mh. Anthony Mavunde na mkono wa kulia Mh. Omary Mgumba Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo Anthon Mavunde ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza Bajeti ya Wizara ya Kilimo kutoka shilingi Bil. 294 kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 hadi shilingi Bil. 954 kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo amebainisha kuwa Wizara hiyo ipo kwenye mipango ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji na tayari wameanza kuyapitia mabonde makubwa 22 hapa nchini yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji na kuyafanyia utafiti ili kujenga miradi mikubwa ya umwagiliaji.
Aidha amesema Wizara imejipanga kuikuza Sekta ya Kilimo kwa kwa asilimia 10 kufikia mwaka 2030 kwa kuongeza uzalishaji katika Kilimo cha umwagiliaji na kuviwezeha vituo vya Utafiti kufanya utafiti wa Mbegu bora, huku mikakati mingine ikiwa ni pamoja na kuziwesha Maabara kupima udongo ambapo kwa kuanzia tayari wameshapima udongo kwa mikoa 18 ya Tanzania ili kuwafanya Wakulima waachane na kilimo cha kubahatisha lakini pia ametoa rai kwa viongozi wa mikoa ya Kanda ya Mashariki kuhakikisha wanatenga maeneo ya kilimo kwa ajili ya vijana na kwamba Serikali ipo tayari kushirikiana nao katika kuhalikisha Sekta ya Kilimo inachangia kupunguza tatizo la ajira nchini na kujenga Maghala kwa ajili ya kuzuia upotevu wa mazao baada ya kuvunwa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa amesema Mkoa umejipanga kukomesha changamoto kubwa ya migogoro ya wakulima na wafugaji na kwamba wanajipanga kutenganisha maeneo ya wakulima na wafugaji ili kukomesha migogoro hiyo lakiniu pia amesema maonesho ya Nanenane ya mwaka huu pamoja na kuwa yamechelewa kuanza yamefanikiwa kutembelewa na wananchi takribani 70,000 kutoka sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi huku yakiwa chini ya kaulimbiu ya ajenda ya 10/30Kilimo ni Biashara, shiriki kuhesabiwa kwa mipango Bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Wa kwanza kushoto Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Yuda Mgeni, Pascal Basiga mshindi wa nafasi ya kwanza mfugaji wa samaki, Hamad Enzi mshindi wa kwanza mkulima bora pamoja na Afisa Kilimo Elina Dastan wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya washindi hao kupokea vyeti vyao.
Katika Maonesho hayo Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa imefanikiwa kujinyakulia nafasi mbalimbali za ushindi ikiwemo nafasi ya kwanza kwa kutoa mkulima bora kwa mkoa wa Morogoro, nafasi ya kwanza kwa mfugaji bora wa samaki kimkoa na nafasi ya tatu kiujumla kwa mkoa wa Mkoa wa Morogoro huku nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Manispaa ya Morogoro na nafasi ya pili Halmashauri ya Mji
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa