Imeelezwa kuwa Mapato yatokanayo na Sekta ya Utalii yanazidi kuongezeka ambapo kwa kipindi cha miezi sita Julai hadi Disemba 2024 shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA limekusanya kiasi cha Shilingi 325,146,978,076.63 sawa na asilimia 75 .5 ya Malengo ya makusanyo ya mwaka.
Hayo yameelezwa leo Januari 25,2025 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia Msemaji Mkuu wa Serikali Bw.Gerson Msigwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka Mikoa ya Morogoro na Dodoma kuhusu utekelezaji wa Serikali katika Hifadhi ya Taifa Mikumi Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro ambapo amesema Serikali imeendelea kuimarisha matumizi ya teknolojia katika kusimamia shughuli za uhifadhi, ukusanyaji wa mapato, utangazaji wa utalii na fursa za uwekezaji ndani na nje ya nchi.
Amesema katika kuhakikisha dhamana hiyo inafikiwa, Serikali kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) imeendelea kutekeleza mambo mbambali ikiwemo Kuhifadhi wanyamapori, bioanuai na makazi ya wanyama katika Hifadhi za Taifa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vya baadae.
Msigwa amesema Shirika limeongeza matumizi ya sayansi na teknolojia katika uhifadhi hasa kwa viumbe adimu na vilivyo katika hatari ya kutoweka ili kuhakikisha ulinzi wao umeimarika na idadi inaongezekana na kwamba wameendelea kuboresha mahusiano na wananchi waishio jirani na Hifadhi kupitia mpango wa ujirani mwema kwa kutoa elimu ya uhifadhi, kutatua migogoro ya mipaka na kushirikiana nao katika maendeleo ya Uhifadhi, ujenzi wa miradi mbalimbali na uboreshaji wa huduma za kijamii.
Pia ameeleza kuwa wamefanikiwa kulipa fidia kwa wakazi zaidi ya 3,500 wa kata ya Nyatwali iliyopo Wilaya ya Bunda Mkoa wa Mara ili eneo hilo liwe sehemu ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti kutokana na umuhimu wake katika ikolojia ya wanyamapori na shughuli za uhifadhi.
Katika uhifadhi na utalii,Msigwa amesemakuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya jitihada kubwa za kutangaza utalii na fursa za uwekezaji nchini na kwamba jitihada hizo zimezaa matunda kwani ameifungua nchi kiutalii na uwekezaji kupitia filamu aliyoiongoza ya “Tanzania: The Royal Tour” na baadae “The Amazing Tanzania” na kusema amesema filamu hizo zimeleta matokeo chanya katika sekta ya utalii na kuchangia ongezeko kubwa la idadi ya watalii, sambamba na ongezeko la uwekezaji na mapato yatokanayo na utalii.
Pia, kumekuwa na ongezeko la safari za ndege za moja kwa moja kutoka maeneo mbalimbali ya dunia kuja Tanzania kupitia mashirika kama KLM, Qatar Airways, Emirates na Turkish Airlines, Amesema utalii kwenye Hifadhi za Taifa umeendelea kukua pia idadi ya watalii na mapato yameongezeka mwaka hadi mwaka.
Aidha amesema kuwa watalii wameengezeka,Idadi hii imeongezeka ikilinganishwa na watalii milioni 1,618,538 waliotembelea Hifadhi za Taifa mwaka 2022/2023 ambalo ni ongezeko la watalii 244,570 sawa na asilimia 15.1. huku kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 Shirika lilikadiria kupokea watalii milioni 1,848,759 ambapo kwa kipindi cha miezi sita Julai – Disemba 2024 watalii milioni 1,146,438 walitembelea Hifadhi za Taifa ambayo ni sawa na asilimia 62 ya makadirio ya mwaka.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa