|
Mwenge wa uhuru 2024, umepokelewa leo Aprili, 2024 wilayani Kilosa ukitokea wilaya ya Gairo na kuanza kukimbizwa na kutembelea, kuzindua na kukagua miradi ya maendeleo kuanzia 22 Aprili, 2024 na kuukabidhi 23 Aprili, 2024 katika wilaya ya Kilombero Kijiji cha Idete.
Mkuu wa wilaya ya kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka amepokea mwenge huo kutoka wa Mkuu wa wilaya ya Halmashauri ya Gairo Mhe. Jabir Omar Makame
Akiongea wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika katika kata ya Mtumbatu wilayani Kilosa Mhe. Shaka amesema kuwa mwenge wa uhuru utakimbizwa umbali wa km 331.9 katika Tarafa sita kati ya saba, kata 21 kati 40 na vijiji 37 kati ya 138 ambapo utapitia jumla ya miradi sita ya maendeleo na shule ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Mhe.Shaka ameongeza kuwa Miradi hiyo ya maendeleo yenye thamani ya shilingi 2,883,413,707.71 (100%) ambapo shilingi 1,800,000,000.00 (0.06%) Mchango wa wananchi, Shilingi 58,772,400.00 (2.04%) Mchango wa Halmashauri, shilingi 967,916,557.29 ( 33.57%) mchango wa serikali kuu, na shilingi 1,854,924,750.42 (63.33%) mchango wa wahisani .
Ameeleza kuwa miradi 4 itazinduliwa, 1 utafunguliwa na 2 kuonwa. Miradi hiyo ipo katika Sekta ya Elimu, Afya, Barabara, Maji, Kilimo na Maendeleo ya Jamii. Ambapo mwenge huo utakimbizwa ndani ya halmashauri ya wilaya ya kilosa na kuitimisha mbio hizo 23 Aprili, 2024 na kukaabidhi wilaya ya Kilombero halmashauri ya Mlimba Kijiji cha Idete.
Mradi uliozinduliwa na mwenge wa uhuru mpaka sasa ni mradi wa ujenzi wa kalavati lenye midomo minne masombawe kata ya mamboya wenye thamani ya shilingi 356,286,300.00 fedha kutoka serikali kuu ambapo mradi huo utasaidia kuondoa kero za wananchi kusafiri umbali mrefu wa zaidi ya kilomita 15 kutoka Mamboya kupitia Magubike pia itachagiza shughuli za kiuchumi.
Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 ni “Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”.
|
|
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa