Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwani Kikwete amewahimiza viongozi wa Wilaya ya Kilosa kusimamia mpango wa matumizi ya mashamba 11 aliyoyakabidhi mwishoni mwa wiki hii kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Ridhiwani ametoa agizo hilo wakati alipofanya ziara ya siku moja ambapo pia amewashukuru wananchi kwa jinsi wanavyoendelea kushirikiana na Rais Samia katika kujiletea maendeleo.
Aidha amesema kuwa Rais ameona kipaumbele kikubwa cha mashamba hayo kiwe ni wananchi ambao amewaomba kujiunga kwenye vikundi vya Ushirika ili kuyatumia kwa ajili ya Kilimo chenye tija.
Nao baadhi ya wananchi walimshukuru na kumpongeza Rais kwa kuwapatia mashamba hayo huku wakiahidi kuyatumia kama walivyoelekezwa.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa