Imeelezwa kuwa pamoja na uhitaji wa ardhi miongoni mwa wananchi kwa ajili ya matumizi mbalimbali kiwemo makazi, malisho ya mifugo pamoja na mashamba wananchi wameshauriwa kuzingatia mpango mzima wa matumizi bora ya ardhi ili kuepukana na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikiibuka mara kwa mara na kusababisha madhara mbalimbali ikiwemo mapigano na kutokuelewana .
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe S. Kebwe wakati alipotembelea kata ya Mvumi katika vijiji vya Gongwe na Mvumi na kuongea na wananchi katika mkutano wa hadhara katika vijiji hivyo ambavyo viko katika mgogoro wa mashamba yaliyofutwa namba 32 hadi 36.
Kutokana na mgogoro huo Mkuu wa Mkoa amemwagiza Afisa Ardhi Mkoa kwa kushirikiana na Afisa Ardhi Wilaya kupitia upya mashamba hayo na kuhakiki ili kuyagawa katika usawa kwa vijiji hivyo viwil,na amewataka wananchi hao kuwa na subira kwa sasa wakati kazi hiyo ikifanyika na kwamba shughuli zote katika mashamba hayo zisitishwe hadi hapo uhakiki utakapokamilika na mashamba hayo kugawiwa kwa wananchi hao chini ya usimamizi wa Mkuu wa Wilaya kwa kufuata utaratibu utakaopangwa.
Pamoja na mgogoro huo wananchi wa vijiji vya Gongwe na Mvumi wamemshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa ajili ya mashamba hayo yaliyofutwa na kwamba kufutwa kwa mashamba hayo kumekuwa na tija kwao kwani kupitia mashamba hayo watapata ardhi ya kulima na hata kupata wawekezaji jambo ambalo litawaingizia kipato katika vijiji vyao na ajira kutoka kwa wawekezaji....
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa