Mwenge wa Uhuru 2021 umekimbizwa wilayani Kilosa Agosti 4 na kufanikiwa kutembelea miradi mitano na kupongeza utekelezaji wake aidha mwenge wa uhuru pamoja na umewapongeza Viongozi wa Wilaya ya Kilosa kwa kufanya vizuri miradi mingine minne iliyotembelewa.Akiongea mara baada ya kukamilika kusomwa kwa Risala ya Utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyosomwa na Katibu Tawala Ndg. Yohana Kasitila, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa LT Josephine Paul Mwambashi amesema Mwenge wa Uhuru haukuweza kuweka jiwe la msingi mradi huo kutokana na kukosa nyaraka za malipo ya ujenzi wake,
Lt. Josephine Mwambashi ametumia fursa hiyo kutoa angalizo kwa viongozi wanaopewa dhamana ya kusimamia miradi ya maendeleo kuwa wazalendo katika kusimamia miradi hiyo kwa kwani Serikali inatoa fedha hizo kwa ajili ya watanzania kupata huduma muhimu zikiwemo za afya, maji, elimu, barabara na huduma nyinginezo katika sekta mbalimbali hapa nchini.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mh.Majid Mwanga amesema kuwa mwenge wa uhuru amepitia miradi ya maendeleo mitano yenye thamani ya zaidi ya Tsh.2.2Bil. ikiwa katika sekta ya Afya, Maji na Elimu ambapo katika utekelezaji wa miradi yote hiyo Serikali kuu imechangia Tsh.1,348,431,600/=, Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kiasi cha Tsh. 470,993,161 na Tsh. 205,295,000 ni mchango kutoka kwa wananchi.
Pamoja na hayo Agosti 5 Mkuu wa Wilaya alikabidhi mwenge wa uhuru wilayani Ulanga mara baadha ya kumaliza mbio zake wilayani Kilosa ambapo alimkabidhi mkuu wa wilaya ya ulanga Mh.Ngollo Malenya mwenge wa uhuru pqamoja na wakimbiza mwenge wote wakiwa salama.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa