Mbunge wa jimbo la Kilosa mjini Mh. Mbaraka Bawazir Mei 4 mwaka huu amechangia vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya ugojwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya Corona ambao umetangazwa kuwa janga la kidunia ambapo amechangia thermoscanner, ndoo 60 za kunawia mikono zikiwa na koki zake, barakoa box 6, gloves pamoja vitakasa mikono box 1 ili viweze kusaidia katika kudhibiti na kupambana na corona.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Wilaya mwakilishi wa Mbunge huyo ambaye ni diwani mstaafu Ahmed Islam Kabuma amesema corona ni janga la kidunia na kwamba ili kuushinda ugonjwa huo ni muhimu kuwa na ushirikiano ambapo kwa upande wake ameahidi kutoa shilingi milioni ili kuchangia mapambano hayo.
Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi amesema anamshukuru mbunge Bawazir pamoja na diwani mstaafu Mh. Kabuma kwa kuonyesha kujali kwani matatizo ya ugonjwa wa corona yanaweza kumpata yoyote hivyo ushirikiano unahitajika kwa watu wote huku akiendelea kuwasihi wadau wengine kuendelea kutoa michango yao mbalimbali ambayo ni msaada mkubwa katika kipindi hiki na kwamba itasaidia katika kujiknga pamoja na kununua madawa mbalimbali ya kujitibia.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi katika kudhibitii corona ametoa mchango wake wa barakoa 400 ikiwa ni sehemu ya mchango wake lakini pia amekabidhi thermoscanner moja iliyotolewa na mdau Mohamed Nassoro pamoja na barakoa ambapo amekabidhi vifaa vyote kwa pamoja kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Asajile Mwambambale kwa ajili ya kufanya kazi iliyokusudiwa.
Aidha kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya imempongeza Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na timu yake kwa jitihada mbalimbali ambazo wamekuwa wakizionyesha katika kuchukua hatua mbalimbali za kupambana na kuhakikisha wilaya ya Kilosa kiujumla na wakazi wake wanachukua hatua stahiki za kujikinga na janga la corona ikiwemo kuhamasisha wadau mbalimbali kutoa michango mbalimbali ya vifaa ili kudhibiti corona.
.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa