Mbunge wa Viti Maalumu anayeshughulikia wafanyakazi Mhe. Dkt. Alice Karungi Kaijage amefanya ziara ya kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kilos ana kusikiliza changamoto, ushauri na mapendekezo ya watumishi wilayani hapo.
Akizungumza 14 Disemba,2023 katika ukumbi wa shule ya msingi Mazinyungu Mhe. Alice amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kusikiliza changamoto, kubaini maendeleo ya watumishi pia kupokea ushauri wa watumishi kwa serikali katika kipindi hiki cha miaka mitatu hususani katika masuala ya kiutumishi.
Ameongeza kuwa ni jukumu lake kuhakikisha anatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa kusimamia vema mambo mbalimbali ya kiutumishi nchini. Ambapo katika kikao hicho watumishi wialayani kilosa waliweza kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili, kutoa ushauri na mapendekezo ikiwemo kuwepo na usawa stahiki katika idara zote na vitengo kama vile kulipwa kwa wakati malipo ya likizo, malipo ya wastaafu, uwepo wa magari na pikipiki katika idara zote na vitengo, nyumba za kuishi watumishi wote, fedha za usimamizi na ufatiliaji wa miradi, kupandisha madaraja, kubadilisha muundo, Pamoja na ongezeko la fedha za matumizi mengineyo (OC).
Mhe. Alice ameongeza kuwa katika kipindi cha mika mitatu Serikali imeweza kupandisha madaraja watumishi 425,000 amabpo kwa mwaka inaigharimu serikali kiasi cha shilingi Tilioni 1.12 lakini pia kwa upande wa ajira takribani watumishi 129,000 kutoka serikali kuu na 21,000 kutoka serikali za mitaa wameajiriwa.
Pia ameeleza kuwa katika bajeti yam waka wa fedha 2023/2024 serikali imeweza kuajiri watumishi 47,000 na kusema kuwa serikali inaendelea kuwajali watumishi wake kwa kubadilisha miundo ya watumishi 3,345.
Katika hatua nyingine Mhe. Alice ameshauri kuwepo na utaratibu wa kufanya vikao na watumishi ili kubaini changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi hao na kuzitafutia ufumbuzi kwa wakati.
Naye kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmasahuri ya Wilaya ya Kilosa Ndg. Joseph Kapere amesema kuwa changamoto mbalimbali za kiutumishi zinaendelea kutatuliwa kulingana na bajeti iliyopo.
Pia ameongeza kuwa fedha ya mapato ya ndani Halmashauri ujiwekea vipambaule ambavyo viko kwenye bajeti na mambo ambayo hujitokeza kwa dharura kama vile mafuriko ambapo Halimashauri ipo katika hali hiyo kwa sasa na kusababisha baadhi ya mambo kutokamilika kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa