Elimu ya mfumo Tausi wa kukata lesen za biashara na kufanya malipo ,kukata vibali mbalimbali na kutoa kodi za Serikali bila kufika katika ofisi husika za halmashauri umeanza rasmi kutolewa kwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro.
Akitoa Elimu hiyo Afisa Biashara Wilaya Idrisa Jukulu kwa wafanyabiashara wa Tarafa ya kimamba na Kilosa amesema mfumo huu ni mfumo mpya ulliotolewa na TAMISEMI utawarahisishia wafanyabiashara wote na wanaolipa ushuru mbalimbali kufanya malipo na kukata lesen sehemu yoyote walipo bila kufika ofisi za Halmashauri kwaajili ya kupata huduma hiyo.
Aidha amefafanua kuwa mfumo huu utaanza kutumika rasmi kuanzia mwezi wa saba mwaka huu ambapo kwasasa umeanza kutumika kwa wateja wapya ambao wanafungua biashara zao ambazo zinahitaji lesen za biashara .
Jukulu amesema mfumo huo unaweza kutumika kupitia simu janja kwa mfanyabiashara ambapo ili kufanikisha kutumia mfumo huo na taratibu nyinginezo mfanyabiashara atatakiwa kuwa na namba ya NIDA yenye majina ya mfanyabiashara husika, TIN namba, namba ya simu ambayo imesajiliwa..
Amesisitiza kuwa mfanyabiashara atakayeomba leseni ya biashara kwa njia ya mfumo wa Tausi anatakiwa kuchagua aina ya leseni ya biashara anayoifanya na kwamba kinyume na hapo ni kosa kuomba leseni tofauti na biashara unayoifanya na kwamba mfanyabiashara yoyote atakayekiuka taratibu hizo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
|
|
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa