Viongozi ngazi ya Vitongoji, Vijiji na Kata wametakiwa kuacha utaratibu wa kuingiza mifugo kiholela katika maeneo yao kutoka miji ya jirani hususani maeneo ya mipakani kwani kufanya hivyo ni kinyume na utaratibu na atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
Hayo yameelezwa Julai 16, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza na wananchi katika Ziara yake kata ya Malolo ambapo amewataka viongozi hao kutimiza uwajibu wao pasipo kutanguliza maslahii yao binafsi kwani kufanya hivyo kunasababisha migogoro ya Wakulima na Wafugaji wilayani hapa.
Mhe. Shaka amesema kuwa viongozi wamepewa dhamana ya kulinda na kutetea maslahi ya wananchi na sio kuwakandamiza kwa kutumia vibaya mamalaka waliyopewa kwa manufaa yao binafsi na kwamba hali hiyo inasababisha uvunjifu wa Amani katika maeneo yao
“Ni marufuku kuingiza mifugo kwenye kata hii na wilaya hii kinyume na utaratibu tukikubaini hatua kali za kinidhamu tutazichukua” . Alisisitiza Mhe. Shaka
Mkuu huyo wa Wilaya ameongeza kwa kusema kuwa asilimia 80 ya shughuli zinazofanyika katika kata hiyo ni kilimo hivyo amewataka Viongozi hao kujikita zaidi katika kusimamia shughuli za kiuchumi zitakazoleta maendeleo kwa Wananchi wa kata hiyo na Wilaya nzima kwa ujumla.
“Mkipata ushauri mzuri wa kitaalamu wa kilimo Malolo mnauwezo wa kufungua fursa za wafanyabiashara wakubwa ndani na nje ya nchi kuja kuchukua bidhaa katika kata hii”. Alisema Mhe. Shaka
Katika Ziara hiyo Mhe. Shaka amembelea na kukagua Miradi ya maendeleo ikiwemo Mradi wa usambazaji wa maji safi na salama, Ujenzi wa barabara kiwango cha kokoto kitongoji cha Ruaha darajani,Shule ya msingi Chabi na kituo cha afya Malolo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa