Kupitia maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara amepongeza namna mjadala wa maendeleo endelevu ndani ya miaka 61 ya Uhuru ulivyofanyika kwani umetoa elimu kwa wanakilosa na watanzania kiujumla kujua juhudi na historia nzima ya upatikanaji wa Uhuru.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Tawala Mkoa Dkt. Mussa A. Mussa, alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro wakati wa Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wilayani Kilosa katika mdahalo ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za miaka 61 ya Uhuru ambapo wananchi walipata fursa ya kuelewa historia ya Uhuru huku akitaka midahalo hiyo kuwa endelevu ili iweze kuwa msaada kwa wananchi kufahamu mambo mbalimbali kuhusu Uhuru namna ulivyopatikana.
Dkt. Mussa amesema kuwa tunapotaja uhuru wa Tanganyika tunaangalia tukio kubwa la kushushwa bendera ya wakoloni na kupandishwa bendera ya Tanganyika pamoja na tukio la kuwasha mwenge wa Uhuru, matukio ambayo yana historia kubwa katika nchi yetu huku akitaka watanzania kuyabeba kwa kina maneno yaliyotamkwa na hayati Mwalimu Nyerere kuwa "Tunataka kuwasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu; ulete tumaini pale ambapo hakuna matumaini; upendo mahali palipo na chuki na heshima palipojaa dharau"ambapo ametaka maneno hayo kueleweka kwa kina kwa watanzania kwani ndio dira ya uhuru.
Aidha katika maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo suala la maadili, uzalendo, historia na umuhimu wa Serikali za Mitaa iliyotolewa na Mbunge wa Mikumi Mh. Dennis Londo huku mada ya Historia ya Uhuru wa Tanzania ikitolewa na Mbunge wa Kilosa Mh. Prof. Palamagamba Kabudi na kuhitimishwa na tukio la utoaji zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari waliofanya vema katika uandishi wa insha juu ya miaka 61 ya uhuru.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa