Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Exaud Kigahe ameitaka Mikoa yote kuanisha maeneo ya uwekezaji na kuyatangaza ili wawekezaji wakifika Nchini wakute mazingira wezeshi kwa kuwekeza na kukuza Utalii na uchumi wa Nchi.
Naibu Waziri huyo amesema hayo septemba 28,2023 wakati wa kufunga maonesho ya KARIBU UTALII KUSINI yaliyofanyika Mkoani Iringa kuanzia septemba 23 mpaka 28 yakishirikisha Mikoa 10 lengo likiwa ni kuhamasisha shughuli za Utalii katika Mikoa ya Kusini ikiwa ni jitihada za kuunga mkono Juhudi za Mhe Rais Dokta Samia Suluhu Hassan za kutangaza Utalii.
Amesema kuwa kila Mkoa na Wilaya uandae mikakati thabiti ya kukuza utalii na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji ambapo ameitaja Mikakati hiyo kuwa ni pamoja na Mikoa na Halmashauri zote kuendelea kutangaza fursa za utalii,Kuibua mazao ya Utalii na kuendelea kutangaza vivutio vya utalii kusini,Timu za uratibu zifanyike kwa pamoja ili kuweza kuandaa kwa ufanisi maonesho ya Karibu utalii kusini.
Sambamba na hayo Naibu Waziri Kigahe amewataka Watanzania kuwekeza katika Hoteli za nyota 5 ili kuweka mazingira mazuri kwa wageni wanaokuja kutalii na wawekezaji hivyo kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa ambao ni wenyeji wa maonesho hayo Mhe Halima Dendego amesema kuwa Mhe Rais Dokta Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara na Balozi katika kutangaza na kukuza utalii hivyo maonesho hayo ya Karibu utalii kusini ni jitihada za kuunga mkono juhudi zake za kutangaza utalii.
Katika Maonesho hayo banda la Wizara ya maliasili na utalii limeibuka kuwa banda bora la jumla na katika mabanda ya Mikoa banda la mkoa wa Njombe limeshika nafasi ya kwanza likufuatiwa na banda la Mkoa wa Morogoro.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa