Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Omary Mgumba ameonyeshwa kuridhishwa na kazi ya maandalizi ya uwepo wa kiwanda cha sukari cha Mkulazi II unaondelea katika kata ya Mbigiri ambapo amejionea kazi nzuri ikiwemo uwepo wa mashamba ya miwa, ujenzi wa nyumba za watumishi, jengo la utawala, uwepo wa vifaa pamoja na ukarabati wa barabara ambayo awali ilikuwa haipitiki.
Mgumba ameonyeshwa kuridhishwa na maendeleo makubwa yaliyofanyika katika kiwanda hicho cha mkulazi II Mei 26 mwaka huu alipokuwa katika ziara yake ya siku moja katika kiwanda hicho ambapo amepongeza kazi kubwa iliyofanyika chini ya Mkulazi pamoja na uongozi wa bodi na kusema kuwa yapo maelekezo yaliyotolewa na Serikali ambayo kwa kiasi kikubwa yametekelezwa lakini pia amepongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kushirikiana na wabia wao ikiwemo NSSF kwa kufanikisha ununuzi na umiliki wa mitambo mbalimbali ambayo itasaidia katika shughuli nzima za uzalishaji sukari kiwandani hapo.
Mgumba ameonyeshwa kuridhishwa na maendeleo makubwa yaliyofanyika katika kiwanda hicho cha mkulazi II Mei 26 mwaka huu alipokuwa katika ziara yake ya siku moja katika kiwanda hicho ambapo amepongeza kazi kubwa iliyofanyika chini ya Mkulazi pamoja na uongozi wa bodi na kusema kuwa yapo maelekezo yaliyotolewa na Serikali ambayo kwa kiasi kikubwa yametekelezwa lakini pia amepongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kushirikiana na wabia wao ikiwemo NSSF kwa kufanikisha ununuzi na umiliki wa mitambo mbalimbali ambayo itasaidia katika shughuli nzima za uzalishaji sukari kiwandani hapo.
Mgumba amesema yapo maendeleo makubwa ambayo yamefanyika ikiwemo kuendelezwa kwa hekta 1300 za shamba lakini pia umefanyika ununuzi wa mitambo itakayotumika kwa ajili ya shughuli za uzalishaji na mashambani lakini pamoja na udhibiti na ujenzi wa daraja pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya umwagiliaji ambayo awali miwa ilikuwa ikiathirika kutokana na ukame lakini kwa sasa kutokana na uboreshaji huo wa miundombinu ya umwagiliaji hali itakayosaidia zaidi ya hekta 700 kunufaika na mbiundombinu hiyo huku akibainisha kuwa utendaji wa Serikali si wa maneno bali kwa matendo ambayo yanadhihirika wazi ikiwemo ujenzi wa kiwanda hicho cha sukari.
Pamoja na hayo Mgumba amesema mradi wa huo ni wa manufaa makubwa kwa Serikali na nchi kiujumla kwani unakwenda kumaliza tatizo la sukari nchini ambako katika kiwando hicho kwa kuanzia utazalisha takribani tani 50,000 za sukari huku upande wa kiwanda kikubwa cha Mkulazi Estate ukizalisha zaidi ya tani 200,000 na matarajio ni kufika 2020/24 kutakuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani 250,000 na kwamba tatizo la sukari litakuwa limeisha nchini kwani jicho la Serikali lipo katika kiwanda cha Mkulazi ikiwa ni kampuni itakayokuwa na uhakika wa kuzalisha sukari yenye utoshelevu nchini.
Akielezea suala la upatikanaji wa mbegu Mgumba amesema kiwanda hicho kina mtambo wa kuchemshia mbegu na kutoa uhakika wa mbegu zinatakazotolewa na kutumika kiwandani hapo ni za uhakika na kuepusha hasara kwa nchi kwani kupitia mapungufu mbalimbali yaliyojitokeza Serikali imejiwekea mikakati ya uhakika kwa kushirikiana na kiwanda hicho kwa kuhakikisha mbegu zenye kuleta matokea mazuri na zitatumika katika uzalishaji na kwamba taratibu sahihi zinafuatwa katika uzalishaji miwa kiwandani hapo kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu kwani hatua zote zinapofuatwa katika kilimo cha miwa hadi kufika kiwandani inachukua miaka mitatu.
Akitoa rai kwa wananchi Mgumba amewataka wananchi na wakulima kiujumla kutumia fursa ya uwepo wa kiwanda hicho kinachotarajiwa kufungwa mitambo mwaka huu kuwa wakulima wasisite kutumia fursa ya uwepo wa kiwanda hicho kwa kulima miwa kwa kiwango cha kutosha kwani soko lipo na kwamba Serikali inaendelea kuwekeza katika kiwanda hicho kwa kuhakikisha mahitaji yote yanapatikana huku akiendelea kuipongeza NSSF kwa kutenga bajeti kwa ajili ya kuendeleza mradi huo ambapo pia amewataka wananchi kuachana na suala la upotoshaji kuwa mfuko kwa ajili ya kiwanda hicho unalegalega kuwa habari hizo si za kweli na kwamba mradi huo upo na una faida kubwa ikiwemo soko la uhakika ndani ya nchi , kuongezeka kwa mapato pamoja na ajira kwa vijana na kwamba uhaba wa sukari unakwenda kumalizika kutokana na uwekezaji unaofanywa na Mkulazi.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa