Katika kuhakikisha watanzania wanakuwa na maisha bora na kufikia uchumi wa kati Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) imewawezesha wakulima wadogo 17 wa mashamba ya miwa kwa kuwawezesha kukopeshwa shilingi milioni 550 baada ya kurasimisha ardhi yao na kupata hati zilizowawezesha kukidhi vigezo na kukopeshwa fedha hizo na Benki ya Maendeleo ya Wakulima Tanzania(TAB) ili kuwasaidia kulima kilimo bora na chenye tija zaidi.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi amebainisha hayo Agosti 21 mwaka huu mara baada ya kukabidhi hati miliki 312 kwa wananchi wa kijiji cha Magubike katika kata ya Magubike wilayani Kilosa ambapo amewataka wananchi hao kuzitunza hati hizo kwani ni sawa na pesa pindi zitakapotumiwa vizuri na kuwakwamua kiuchumi na kwamba licha ya benki ya TAB zipo benki nyingine zinazofanya hivyo na zimeonesha nia ya kusaidia wakulima wenye hati ili kukua kiuchumi .
Aidha Mgoyi ametoa rai kwa wananchi ambao wameshafanyiwa upimaji ardhi na kuwa na mpango bora wa matumizi ya ardhi kutumia fursa ya umiliki wa hati hizo kuondokana na umaskini kwani uwepo wa hati hizo unaepusha migogoro ya ardhi na unampa mmiliki fursa ya kupata mkopo,unaongeza uwepo wa amani na mmiliki kujikomboa katika umaskini na unyonge.
Pamoja na hayo Mgoyi ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kutenga fedha kwa ajili ya kusaidia upimaji ardhi ambao utasaidia kuwepo kwa matumizi bora ya ardhi jambo litakalowasaidia kuwepo kwa matumizi ora ya ardhiambapo wananchi wengi watanufaika na hati hizo.
Naye mratibu wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Bi. Seraphia Mgembe amewataka wakurugenzi nchini kuwasaidia wananchi kwa kuwaunganisha na taasisi za kifedha ili wapate mikopo ambayo itawasaidia kuinuka kiuchumi sawa na kuwa na maendeleo ili kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais wa Tanzania za kufikia uchumi wa kati kwa watanzania.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa