Madaraja manne yamesombwa na maji huku watu zaidi 300 wakikosa makazi kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Wilayani kilosa Mkoani Morogoro na kupelekea mafuruko katika mito ya Mkondoa,Ilonga na Mazinyungu kujaa maji.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mkuu Mhe Adam Khigoma Malima baada ya kutembelea maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa na mafuriko hayo na kuwataka Tanroads kurejesha mawasiliano ya Barabara zilizofungwa kwa haraka ili kuwezesha shughuli za kiuchumi kuendelea.
Kufuatia Mvua kubwa iliyonyesha wilayani hapa na mikoa jirani usiku wa kuamkia Disemba 10 mwaka huu 2023 madaraja manne yameharibiwa na yamefungwa kutumika ikiwemo daraja la mto Mazinyungu,Mkondoa na Ilonga.
Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Mhandisi Razack Kyamba amesema kuwa tayari wameshafanya tathmini ya athari iliyopo na kwamba watarejesha Mawasiliano ya Barabara ya Dumila-Kilosa ndani ya siku mbili.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa