Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa kazi kubwa inayofanywa na Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inaongeza kasi ya maendeleo na nchi kukua kiuchumi.
Mhe Shaka amesema hayo baada ya kumalizika kwa kongamono la uwekezaji akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mhe Adam Malima ambapo ameeleza mkakati wa usambazaji wa Umeme ifikapo Juni mwaka 2024 huduma ambayo ni muhimu kwa maendeleo hususan katika kuvutia uwekezaji mkubwa.
Amesema kazi kubwa inayofanywa na Serikali katika kufanikisha maendeleo ya Wananchi na Taifa kwa ujumla inapaswa kuungwa mkono na kila mmoja ili dhamira ya kupaisha uchumi wa nchi ifikiwe kwa haraka huku wananchi wakinufaika na fursa.
Aidha amesema kuwa Tanzinia ni moja kati ya Nchi 10 za Afrika zinazokuwa kwa kasi kiuchumi kwani kwa miaka kumi iliyopita Uchumi wa Nchi ulikuwa kwa wastani wa asilimia saba,ambapo Julai 2020 ,Benki ya Dunia (WB) ilipaisha Tanzania kuwa Nchi ya Uchumi wa kipato cha mwanzo cha kati.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa