Katika kuhakikisha inaunga mkono juhudi za Serikali mradi wa fursa kwa vijana awamu ya pili (OYE II) unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV) pamopja na mashirika zawa ikiwemo MJUMITA umekabidhi vifaa mbalimbali vijana walio chini ya mradi wa fursa za ajira kwa vijana wa awamu ya pili kwa lengo la kuwawezesha kujikwamua kwa kuwapatia vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi 34,468,000 ili kuwasaidia vijana hao kujikwamua kiuchumi.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Kamanda wa TAKUKURU Gwakisa Gwamaka amewataka vijana hao waliopata mafunzo katika maeneo mbalimbali kutumia vifaa hivyo kwa kuchochea maendeleo yao na wilaya kiujumla ikiwemo kujitambua nafasi zao katika jamii na kuwa wabunifu kupitia shughuli zao kwani inategemea kuwaona kuwa chachu njema kwa vijana vingine na kuwa kichocheo kwa wafadhili ili kuleta miradi mingine itakayosaidia vijana wengine zaidi.
Aidha ametaka vifaa hivyo kutunzwa kwa umakini mkubwa ili viwezwe kudumu na kuzalisha zaidi kwani kwa utunzaji huo vitazidi kuleta matokeo chanya na kwamba matarajio ni kuona uwepo wa nidhamu ya matumizi ya fedha zitakazopatikana kupitia shughuli zao lakini pia kuweka akiba ambayo itawasaidia kuongeza vifaa vingine na kukuza pato lao.
Akibainisha vifaa vilivyokabidhiwa Mratibu wa Sughuli za mradi fursa za ajira kwa vijana Hamza Mkomolwa amesema vifaa hivyo ni mizinga ya nyuki 10, mashine 4 za kutengenezea majiko, mashine 2 kubwa na ndogo moja za kutotoleshea mayai, solo 5, viriba rola 2 na birika 2 za kumwagilia vifaa vya kufanyia kazi ya urembo ikiwemo dryer 9, madawa ya kilimo na mifugo pamoja na mbolea ambapo vifaa hivyo vitatumika na vijana hao ambao tayari wamepata mafunzo.
Aidha kwa upande ukaguzi wa fedha za Serikali Halmashauri kupitia mkaguzi wa ndani kwa kushirikiana na mkaguzi toka MJUMITA ilifanya ukaguzi wa fedha za Serikali kwa lengo la kufanya tathmini ya utawala bora kwa vijiji vya Kitunduweta, Chabima, Ulaya Mbuyuni, Unone na Ihombwe vinavyomiliki misitu ya jamii ili kutathmini na kuthibitisha uimara wa mifumo ya uthibiti wa ndani wa usimamizi wa fedha za kijiji, usimamizi wa misingi ya utawala bora kwa kwa kuhakikisha kuwa sheria , kanuni na miongozo inazingatiwa.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa