MVIWATA ngazi kati ya Morogoro ni moja ya mitandao ya ngazi za kati za MVIWATA ambayo ilianzishwa kwa lengo la kuimarisha mawasiliano kati ya vikundi, mitandao ya msingi, taasisi na mashirika wenza yanayofanya kazi na wakulima wadogo ndani ya mkoa wa Morogoro ili kuwezesha kutatua changamoto zao kwa pamoja kama vile kutokuwa na uwakilishi wa wakulima katika vyombo vya maamuzi, kukosa sauti ya pamoja ya wakulima na changamoto za kiuchumi kama vile ukosefu wa masoko ya uhakika na huduma za kifedha na uhakika na usalama wa chakula.
Hayo yamebainishwa na Mratibu wa MVIWATA ngazi ya kati mkoa wa Morogoro Joseph Sengasenga wakati wa utambulisho wa Mradi wa PSA unaofadhiliwa na SDC kupitia Action Aid Tanzania ambapo utakuwa unatekelezwa na MVIWATA ngazi ya kati kwa wilaya ya Kilosa kwa mda wa miaka minne kuanzia 2019 Julai hadi 2023 June ambapo lengo la mradi kuboresha uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali za umma katika maeneo ya huduma za afya ya uzazi na ukimwi kwa vijana wa kike na kilimo kwenye huduma za ugani kwa wanawake ambazo ni za ikolojia, endelevu na salama kwa ajili ya usalama wa chakula katika nchi tano za SADC.
MKURUGENZI MTENDAJI ASAJILE MWAMBAMBALE AKIPOKEA ZAWADI YA KIKOMBE PAMOJA NA DIARY KUTOKA KWA MENEJA WA PROGRAMM KUTOKA UMATI BIVIOLETH ALPHONCE
Sengasenga amesema mradi huo utahusisha sekta ya Afya chini ya UMATI ambayo itakuwa ikiongoza upande wa afya kwenye huduma za afya ya uzazi na ukimwi kwa vijana wa kike huku upande wa sekta ya Kilimo mhusika ni MVIWATA ngazi ya kati Morogoro ambapo itajikita kwenye utolewaji wa huduma za ugani kwa wanawake ambazo ni za ikolojia, endelevu na salama kwa ajili ya usalama wa chakula.
BAADHI YA WATAALAM WALIOSHIRIKI KIKAO HICHO
Aidha amebanisha kuwa vipaumbele vya mradi huo ni Usalama wa chakula ambayo itahusisha Utolewaji wa ajira kwa wagani kulingana na Miongozo/Sera, Ubora wa utolewaji wa huduma za ugani unakidhi vigezo na unatatua changamoto za wakulima wanawake katika kuboresha uzalishaji, Kufanya majaribio ya Kilimo endelevu cha ekologia kupitia mashamba darasa ambapo kata zitakaotekeleza mradi huo ni Mvumi(Kata ya Kitete Kijiji cha Madudu), ILonga, Rudewa, Ulaya na Mhenda ambapo walengwa wa mradi huo wakiwa ni wakulima wadogo wanawake na vijana ambao watajengewa uwezo wa ufatiliaji wa matumizi ya umma katika huduma za ugani.
Akizungumzia upande wa zana ya SAM Sengasenga amesema ni zana ya ufuatiliaji inayomwezesha mwananchi,kamati au kikundi kufuatilia rasilimali za umma,kuanzia pale zinapotoka huku ikilenga kukuza utawala bora hasa katika kufanikisha uboreshaji upatikanaji wa huduma bora, kuhakiki utendaji wa viongozi wa serikali na mamlaka husika, kuboresha na kuimarisha dhana ya uwajibikaji na kuhakiki uwepo wa mipango na utekelezaji wake lakini pia amesema SAM katika ufuatiliaji wa rasilimali za umma husaidia kuwapa wananchi mbinu mbalimbali za kuhoji na kuchukua hatua pale inapoonekana rasilimali za umma hazitumiki kama inavyotakiwa pia inasaidia kupata majibu ya maswali, na mara nyingi, hutoa picha ya namna ambavyo rasilimali husika zimetumikaje na husaidia uboreshaji wa utoaji huduma bora kwa wananchi, kukuza uwajibikaji kwa ngazi mbalimbali, inakuza uzalendo na usawa kwa makundi mbalimbali katika jamii na mwisho huhamasisha wanajamii kupenda, kulinda na kutunza rasilimali za nchi yao kupitia mikutano ya uwezeshaji ambayo huwapa maarifa na mbinu ya namna bora ya kulinda rasilimali za nchi kwa faida yao na vizazi vijavyo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Asajile Mwambambale ametoa rai kwa taasisi mbalimbali zinazofanya kazi na serikali kuutambua vema mfumo wa utendaji kazi wa serikali ili ziweze kufanya kazi na Serikali namna inavyostahiki jambo litakalosaidia kutokuwa na malalamiko kwani mara nyingi kumekuwa na hulka ya taasisi binafsi kufanya kazi na Serikali kama wakaguzi na kukagua namna Serikali inavyofanya kazi na kuikosoa pasipo kujua utendaji kazi wake hivyo kupelekea jamii kupokea taswira tofauti kuhusu utendaji kazi wake hivyo ni vema mfumo wa utendaji kazi ukaeleweka vema ili ushirikiano baina ya taasisi hizo na Serikali ukaleta tija katika jamii .
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa