Wilaya ya Kilosa leo 19 Aprili 2025 imekabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Wilayani Gairo, baada ya kukamilisha ziara ya siku moja,ya kuzindua, na kuweka mawe ya msingi katika miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.8.
Awali katika mkesha wa Mwenge wa Uhuru uliofanyika katika viwanja vya Kilosa Town, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mhe. Shaka Hamdu Shaka, aliwasilisha taarifa ya huduma zilizotolewa usiku wa kuamkia Aprili 19, 2025 na kueleza kuwa watu 219 walipimwa virusi vya UKIMWI, ambapo wanaume wawili na mwanamke mmoja wamegundulika kuwa na maambukizi. A
Mhe Shaka pia amesema watu 201 walipimwa malaria, na wanawake wawili walikutwa na ugonjwa huo na katika kampeni ya uchangiaji damu, lengo lilikuwa kupata chupa 140, lakini chupa 157 zilikusanywa, sawa na unit 112.14.
Aidha Mhe Shaka ameongeza kwa kusema kuwa, watu 29 waligundulika kuwa na uzito uliopitiliza na akatumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi kwa ushiriki wao na kumpongeza Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara wa mapambano dhidi ya UKIMWI, malaria, na lishe duni.
Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndg. Ismail Ali Ussi, ametoa pongezi kwa viongozi wa serikali, vyama vya siasa, na wananchi wa Kilosa kwa mapokezi mazuri na ushirikiano waliouonesha katika shughuli za Mwenge wa Uhuru huku akisitiza umuhimu wa kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa ili kuharakisha maendeleo katika wilaya ya Kilosa.
Kwa sasa, Mwenge wa Uhuru unaendelea na mbio zake katika Wilayani Gairo utazindua na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, huku ukiendelea kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo na uchaguzi mkuu ujao na April 20 utakabidhi kwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro, ambapo makabidhiano ya kimkoa yatafanyika pia.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa