Katibu Tawala Wilaya ya Kilosa Yohana Kasitila ameushukuru uongozi wa benki ya NMB kwa kuonesha ushirikiano na kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Halmashauri ya wilaya ya Kilosa katika kuwaletea maendeleleo wananchi wa Wilaya ya Kilosa.
Afisa tawala huyo ametoa Shukrani hizo oktoba 5 mwaka huu wakati akipokea vitanda na magodoro kumi vilivyotolewa na benki hiyo tawi la Kilombero kwa ajili ya kituo cha afya Mikumi .
Amesema kuwa benki hiyo ni mshirika mkubwa wa maendeleo kwani imekuwa ikitoa michango mbalimbali katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu,afya, na sekta nyinginezo hivyo amesema msaada huo utasaidia katika utoaji huduma kwa wananchi.
Akikabidhi vitanda hivyo na magodoro Katibu na Mkuu wa Idara ya sheria NMB Lilian Komwihangiro amesema benki hiyo inao wajibu wa kuunga mkono juhudi za Serikali na kwamba wanaamini kupitia vifaa hivyo vitakuwa msaada kwa jamii ambao ndio wateja wao.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa