Sera ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli ni kujenga uchumi wa viwanda na kwamba ili kuhakikisha sera hii ya kuwa na uchumi wa viwanda inafanya kazi wadau mbalimbali wa kilimo wilayani Kilosa na hasa idara ya Kilimo Ushirika na Umwagiliaji wametakiwa kuongeza nguvu ya uzalishaji kwani kilimo kwa asilimia kubwa huchangia pato kubwa hapa nchini.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi wakati wa kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango Mkakati kwa mwaka 2017/2018 ambapo mpango huo umepangwa kukamilika ifikapo 2020 ambapo amesema kuwa Halmshauri ina wajibu mkubwa katika kutimiza mpango huo kwa kuongeza juhudi za uzalishaji utakaosaidia kupata mapato ya ndani yatakayosaidia kuhudumia wananchi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Asajile Mwambambale ameitaka bodi ya pamba kuwa na mawakala wengi wanaosambaza viuatilifu vya pamba ili Halmashauri iweze kuwa na wigo mkubwa wa kuchagua kampuni wanayoitaka kuliko hali ilivyo sasa ya kuwa na kampuni moja tu ambayo imepekekea kujitokeza kwa changamoto ya ucheleweshaji wa pembejeo za kilimo na nyingine kushindwa kufanya kazi ipasavyo,ambapo pia ametaka utaratibu wa kupima sucrose kwenye miwa ufanyike kwa uwazi kati ya kiwanda na wakulima sambamba na ushirikishwaji wa wakulima ili kufanikisha utendaji wa haki.
Aidha Mkuu wa Idara ya Kilimo Wilaya Tatu Kachenje amesema kuwa mpango wa kuboresha kilimo una lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara kwa eneo kupitia mnyororo wa thamani ifikapo 2020 ambapo katika utekelezaji wake kwa mwaka 2017/2018 eneo lililolimwa mwaka huu limeongezeka na kufikia hekta 252,799.8 ya eneo la hekta 417,210 linalofaa kwa kilimo ambapo nguvu kubwa kwa msimu uliopita ilitumika katika kuhamasisha na kuelimisha jamii katika mazao mbalimbali yakiwemo ya chakula, mazao ya kimkakati kama vile pamba, korosho na miwa.
Pamoja na utekelezaji huo Kachenje amesema walikutana na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba na kuchelewa kwa mvua, kutokea kwa mafuriko, uwepo wa visumbufu vya mazao,migogoro ya wakulima na wafugaji,uhaba wa vitendea kazi, baadhi ya viuatilifu vya pamba kutofanya kazi vizuri, ubovu wa miundombinu na mbegu bora ya miwa kutopatikana kwa mtiririko mzuri.
Kachenje amesema mpango huo umelenga ifikapo Juni 2018 uwe umeongeza uzalishaji wa mazao ya chakula,uzalishaji mazao jamii ya mizizi, kuimarisha mbinu za uhifadhi wa mazao baada ya mavuno, kuongeza uzalishaji mazao ya biashara, kuboresha kilimo cha mboga mboga na matunda, kuboresha mfumo wa masoko kwa mazao ya kilimo, kuongeza uzalishaji wa mbegu daraja la kuazimiwa ubora kupitia vikundi, kuboresha eneo la umwagiliaji, kuimarisha vikundi 10 vya umwagiliaji katika uendeshaji na utunzaji wa miundo mbinu ya kilimo, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kuimarisha mbinu bora za kuboresha afya ya udongo na kuanzisha majukwaa ya mazao ya biasha
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa