Katibu Tawala Mkoa Ndg. Clifford Tandari Septemba 12 mwaka huu ametoa rai kwa Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kuongeza wigo wa kufikiri lengo ikiwa ni kiongeza kiwango cha ukusanyaji mapato wilayani humo.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wakati wa kikao chake na watumishi hao ambapo amewataka watumishi kutambua kuwa kila mtu ana wajibu katika ukusanyaji mapato ikiwemo kuhakikisha vyanzo vya mapato vinabainishwa na kusimamiwa vema ili mapato hayo yaweze kupanda kwa asilimia nyingi ili yaweze kuleta mabadiliko kwa kuleta maendeleo ili kwenda sawa na kauli mbiu ya wilaya kuwa Kilosa mpya inawezekana.
Aidha ameitaka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwa kushirikiana na Wakuu wa Idara na Vitengo kuhakikisha wanasimamia fedha yoyote inayoletwa na serikali ama inayokusanywa na Halmashauri ili fedha hizo zitumike kama inavyostahili kwa mujibu wa taratibu zinavyoeleza ili kuepuka udanganyifu ama kuchakachuliwa hasa katika mchakato wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa majengo mbalimbali ya Halmashauri, uchimbaji visima, uwezeshwaji wa kaya masikini TASAF na miradi mingineyo inayofanyika katika Halmashauri.
Naye Katibu Tawala Msaidizi anayeratibu masuala yahusuyo Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro Ndg Noel Kazimoto amewataka watumishi hao ili kufanikiwa ni lazima kila mtumishi afanye kazi kwa uadilifu, uaminifu, kujali, kujituma na kufuata misingi, sheria, kanuni na taratibu za kazi ili Halmashauri iwe na maendeleo na kuepuka migogoro ambayo inaweza kuepukwa endapo watumishi wote watajituma na kuwa na nidhamu ya kazi pamoja na kujiheshimu nyakazi zote.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa