Imebainika kuwa mafunzo ya wawezeshaji wa uboreshaji wa opras kwa walimu ngazi ya wilaya kwa waratibu elimu kata wakuu wa shule na walimu wa kuu yamefanyika wilkayani Kilosa lengo ikiwa kuboresha opras kwa walimu ili kuleta mabadiliko ya utendaji kazi katika utumishi wa umma ili kuinua kiwango cha ufaulu.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Paula Nkane ambapo amesema mafunzo yameendeshwa na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwa wawezeshaji hao kwa ngazi ya Wilaya ambapo baada ya mafunzo hayo washiriki watawajibika kuwafundisha walimu madarasani jinsi ya kujaza opras iliyoboreshwa ambayo ni mpango wa kitaifa unaosimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), TSC, PS3 na PS3FP.
Paula amesema kuwa mafunzo hayo yameendeshwa na wataalam toka Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ambao ni Afisa utumishi Wilaya, Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari, Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi na Katibu wa TSC.
Akitoa mafunzo hayo Afisa Utumishi Wilaya Noel K. Abel amesema kuwa opras ni utaratibu wa kumpima mtumishi utendaji kazi wake kwa kipindi cha mwaka mmoja ambao hufanyika kwa uwazi na kwa kufuata utaratibu ambao umebuniwa ili kumsaidia mwajiri na mtumishi katika kupanga mipango ya utekelezaji.
Abel amesema kuwa opras ina faida nyingi kwa mtumishi na mwajiri wake ambapo miongoni mwa hizo ni mtumishi kupata hamasa ya kutekeleza malengo yake kwa ufanisi zaidi na kuwa na uboreshaji wa utendaji endelevu kwani utendaji huo unatambulika na menejimenti huku mwajiri akipata nafasi ya kujikita zaidi katika utekelezaji wa malengo ya taasisi, anafahamu jinsi ya kutoa tuzo ama adhabu kulingana na sifa na utendaji kazi wa mtumishi.
Akibainisha sifa za opras abel amesema opras ina sifa muhimu ambazo zinaweza kutofautishwa kiurahisi ikilinganishwa na mfumo wa siri wa kupima utendaji kazi kwa mtumishi kwani inazingatia uwazi, ushirikishwaji, uwajibikaji na umiliki.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa