Mtandao wa CAMA umekuwa ni msaada mkubwa kwa wasichana mbalimbali ambao wamekuwa wakifadhiliwa na CAMFED ambayo imekuwa ikijishughulisha na kuwafadhili wasichana wanaoishi katika mazingira hatarishi lengo ikiwa ni kuwasaidia kufikia malengo yao hususani katika masomo na stadi mbalimbali za maisha.
Hayo yamebainishwa na Grace Stephano ambaye ni mmoja wawezeshaji wa progam ya Dunia Yangu Bora ambayo inalenga kuwasaidia wanafunzi wakike na wakiume ili waweze kujitambua, kujiamini, kupunguza utoro mashuleni na kupenda Elimu kwa kuhakikisha anafikia malengo yake shuleni lakini pia kuweza kuyafikia malengo yake ya kimaisha.
Akieleza zaidi namna program ya Dunia Yangu Bora inavyofanya kazi Frida Msongamwanja ambaye ni mmoja wa wawezeshaji wa program hiyo amesema program hiyo inafundishwa kwa wasichana waliofadhiliwa na CAMFED ambapo wataipeleka Elimu hiyo mashuleni kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi kupunguza utoro mashuleni, kuongeza ufaulu kwa wanafunzi, kujifunza stadi za maisha ambapo wawezeshaji watapangiwa shule za sekondari zenye mradi wa camfed ili kutoa elimu na kuwasaidia wanafunzi.
Kwa niaba ya wana cama wenzao Christina Mwihuva na Amina Richard wamesema kupitia program ya Dunia Yangu Bora wamejifunza mambo mbalimbali ikiwemo kujithamini, kujitambua na kuwa mfano wa kuigwa katika jamii na kwa wanafunzi kimatendo, mwenendo pamoja na kuwasaidia kubadilika kutoka kwenye mfumo hasi kuelekea mfumo chanya lakini pia namna ya kujikimu kimaisha kwa kujiajiri badala ya kubweteka na kusubiri kutafutiwa hususani kwa watoto wakike kwani maisha kwa sasa yamebadilika.
Aidha wamesema kuwa wanaamini kupitia program hiyo na mafunzo hayo ya siku tisa waliyoyapata italeta badiliko kubwa katika maisha yao na kwa wanafunzi wanaotarajia kuwafundisha kwani itamsaidia mwanafunzi kujiamini, kujitambua, kujithamini na kupenda masomo jambo litakalosaidia kuongeza ufaulu mashuleni lakini pia hata wanafunzi watakapomaliza masomo watakuwa na elimu ya stadi za maisha ambayo itakuwa msaada kuwawezesha kujikimu kimaisha kwa kujiajiri badala ya kukaa bila shughuli yoyote.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa