Katika kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuhakikisha kila wanafunzi wanaendelea vema na masomo na kumaliza vema elimu yao CAMFED imekuwa ikiendesha program ya Dunia Yangu Bora mashuleni programu inayolenga kumsaidia mwananfunzi kujifunza mambo mbalimbali na kuhakikisha pindi mwanafunzi anapomaliza elimu yake anakuwa na uwezo wa kujitegemea na kuwa mwanajamii wa kuigwa.
Akieleza utekelezaji wa program hiyo mashuleni kupitia waongozaji wa wanafunzi waliofadhiliwa na CAMFED Mratibu wa CAMFED Wilaya ya Kilosa Zamoyoni Selemani amesema program hiyo hufundishwa kwa wanafunzi kupata elimu ya stadi za maisha imekuwa chachu ya kuwafanya wanafunzi kupenda shule jambo linalosaidia kupenda shule lakini pia imesaidia kupunguza utoro mashuleni na uwepo wa mimba.
Wakizungumzia mrejesho wa program ya Dunia Yangu Bora upande wa mafanikio waongozaji wa wanafunzi wamesema imekuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi na jamii kiujumla kwani imesaidia kupungua kwa kiwango cha utoro mashuleni, kiwango cha mimba kimepungua, walimu katika shule husika na wazazi/walezi wamekuwa wakitoa ushirikiano lengo ikiwa ni kihakikisha wanafunzi wanahudhuria mashuleni lakini pia wao kwa nafasi ya waongozaji wanaheshimika na kuaminika katika jamii kwa kushirikishwa katika shughuli za kimaendeleo na vikao vya kimaamuzi.
Upande wa changamoto wamesema baadhi ya walimu wamekuwa na mwamko mdogo kutoa ushirikiano kwa waongozaji wa wanafunzi na kutochukulia uzito program hiyo kwa kuona haina tija kwa wanafunzi na jamii, lakini pia baadhi ya wazazi na jamii imekuwa ikitoa ushirikiano mdogo pindi mwanafunzi anapopata ujauzito kwa kuhofia kugundulika endapo watatoa ushirikiano kwa kuweka wazi wahusika huku wakitoa ushauri kwa wakuu wa Idara ya Elimu Msingi na Sekondari kuendelea kutoa elimu kwa walimu walio chini yao kwa kuwapa elimu ya umuhimu wa program hiyo ili wafahamu tija yake kwa jamii na wanafunzi kiujumla.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa