Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi kutunza mazingira na miundombinu ya daraja la Berega ili litumike kwa muda mrefu.
Rai hiyo ameitoa 2 Agosti, 2024 katika kata ya Berega wakati akizungumza na wananchi baada ya kuzindua Daraja hilo lililogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 7.9 fedha kutoka serikali kuu.
Aidha Rais Samia amewasisitiza wananchi kuacha uchimbaji wa mchanga pamoja na matumizi mabaya ya Mto wa Berega ili kutunza kingo za Mto huo.
Mhe. Rais akizungumzia manufaa ya Daraja hilo ambalo limeweza kusaidia kuwaunganisha wananchi na kurahisisha upatikanaji wa huduma za jamii ikiwemo usafirishaji wa mazao kwani magari sasa yatapita kwa urahisi.
Pia Mhe. Rais ameipongeza Wizara ya Tamisemi kwa kazi kubwa ya uendelezaji wa miundombinu kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), wataalamu na wakandarasi waliohakikisha mradi unakamilika.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa