Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adamu Malima amewaomba wadau kuendelea kuwachangia waathirika wa mafuriko wilayani Kilosa kwani Bado wanahitaji misaada mbalimbali.
Mhe. Malima ameyasema hayo Disemba 22, 2023 katika hafla maalumu ya kupokea ripoti ya tathmini ya athari za mafuriko iliyofanyika katika ukumbi wa MT Mjini Kilosa na kuwakutanisha viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge wawili wa Jimbo la Kilosa prof. Palamagamba Kabudi na Mhe. Denis Rondo ambaye ni mbunge wa Jimbo la Mikumi.
Mhe. Malima amesema kuwa misaada yenye thamani ya zaidi ya milioni mia mbili imekusanywa na kugawiwa Kwa waathirika wa mafuriko hayo ikijumuisha vifaa vya ndani, nguo, magodoro, mashuka mikeka pamoja na vyakula.
Ameongeza kuwa Bado milango Bado ipo wazi Kwa wale wenye Nia ya kuwachangia waathirika hao ambapo utaratibu uliopo ni kuwa michango hiyo hukusanywa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambaye ni Mwenyekiti wa maafa wa Wilaya.
Akiwasilisha ripoti hiyo Kwa mkuu wa Mkoa, mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa zaidi ya bilioni mbili zinahitajika Ili kujenga upya Miundombinu iliyoharibiwa na mafuriko hayo zikiwemo Barabara, madaraja, vyoo na marekebisho ya miundombinu ya maji.
Ameongeza kuwa kamati iliyofanya tathmini hiyo inashauri mamlaka kuweka alama za tahadhari maeneo yote ya hifadhi za maji na barabara.
Kwa upande wao wabunge wawili akiwemo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi ambaye ni mbunge wa Jimbo la Kilosa na Mhe. Denis Rondo ambaye ni mbunge wa Jimbo la Mikumi wamewata wenye mamlaka kutafuta suluhisho la kudumu ikiwa ni kutoa Elimu Kwa wananchi Ili waache kufanya shughuli za kilimo na kujenga kwenye hifadhi za mito.
Awali mkuu wa Mkoa huyo amefanya ziara katika maeneo yaliyoathirika na mafuriko lakini pia madaraja yanayotengenezwa na Yale yanayoathirika na mafuriko likiwemo daraja la Dumila, Ilonga, mazinyungu na la moto Mkondoa na kutaka mamlaka za maji Bonde la maji Wami-Ruvu pamoja na TANROADS kujenga mabwawa ya kuvuna maji ya mito hiyo Ili yatumike kwenye shughuli za kilimo,Aidha amewataka wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu katika Kingo za mito.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa