Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewataka waajiri Mkoa wa Morogoro kuendelea kutatua changamoto za wafanyakazi wao ili kuleta mabadiliko mahali pa kazi kwa maslahi mapana ya wafanyakazi na Taifa zima kwa ujumla.
Wito huo umetolewa Mei 1, 2025 wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani yenye kaul;I mbiu isemayo “Uchaguzi Mkuu 2025, Utuletee viongozi wanaojali haki na maslahi ya wafanyakazi sote tushiriki”. Maadhimisho hayo yamefanyika uwanja wa Jamhuri ulipo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Mhe. Malima amesema kuna umuhimu wa waajiri kuwajali na kuwathamini wafanyakazi waokwa kuwatatulia changamoto wanazokumbana nazo ili kuweza kuwapa motisha ya kufanya kazi kwa bidii na kuiletea Taasisi husika husika maendeleo.
“Nichukue fursa hii kuwaelekeza waajiri wote wa sekta binafsi katika mkoa wa morogoro kutatua changamoto za wafanyakazi wao “Amesisitiza Mhe. Adam Malima
Aidha, Mhe. Malima ameitaka Ofisi ya Afisa Kazi Mkoa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye maeneo ya kazi ili kujiridhisha kama mikataba ya wafanyakazi inazingatia sheria za kazi na kubaini wanaovunja sheria.
Sambamba na hayo Mkuu huyo wa Mkoa amewataka viongozi wa OSHA Mkoani umo kuhakikisha wanashughulikia malalamiko ya wafanyakazi na kuwachukulia hatua zaq kisheria waajiri wote wanaokiuka misingi ya kisheria na kukomesha baadhi ya tabia za waajiri kukiuka na kuwakandamiza wafanyakazi.
Kwa upande wa wafanyakazi kupitia risala iliyosomwa mbele ya mgeni rasmi , wameiomba serikali kushughulikia changamoto zikiwemo madai mbalimbali ya wafanyakazi yakiwemo yanayohusu likizo, uhamisho, matibabu, kukaimu, kujikimu,stahiki za ajira mpya na malimbukizi ya mishahara.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa