Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amekemea vikali kitendo kilichoonyeshwa na wanyeviti wa vitongoji 21 katika mamlaka ya Mji Mdogo Mikumi kwa kushindwa kuhamasisha wananchi kushiriki katika ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa katika shule ya sekondari Mikumi ambapo amemuagiza Mkuu wa polisi wilaya ya kipolisi Ruhembe(OCD) kuwaweka ndani wenyeviti hao kwa kuonyesha lengo la kutofanikisha ujenzi wa madarasa hayo ambayo yanategemewa kutumiwa na wanafunzi wanaotarajia kuanza kidato cha kwanza shuleni hapo.
MKUU WA MKOA WA MOROGORO LOATA OLE SANARE
Agizo hilo limetolewa Januari 6 mwaka huu wakati alipokuwa katika ziara yake wilayani Kilosa ambapo amesema ziara yake hiyo ni katika utekelezaji wa agizo la Serikali lililotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa la kutaka wanafunzi wote waliofaulu mitihani ya darasa la saba kuwa madarasani pindi shule zitakapofunguliwa Januari 11, hivyo kila mkoa unapaswa kuhakikisha wanafunzi hawakosi vyumba vya madarasa pamoja na viti na meza vya kukalia.
MBUNGE WA JIMBO LA MIKUMI MH. DENNIS LONDO
Loata amesema shule hiyo inatarajiwa kupokea wanafunzi 432 ambao wamepangwa katika shule hiyo hivyo ametaka kasi ya ujenzi kuongezeka iwemo kufanyika jitihada za kumaliza ujenzi huo kadri inavyowezekana na kwamba hatarajii wanafunzi hao kukosa madarasa ya kusomea huku akitaka wenyeviti hao baada ya kukamatwa wafikishwe eneo la ujenzi kushiriki wao wenyewe katika kazi ya ujenzi kwani wameshindwa kuhamasisha walio katika maeneo yao na kwamba atapita eneo hilo kwa ajili ya ukaguzi wa utekelezaji wa agizo hilo.
BAADHI YA VIONGOZI WA WILAYA, HALMASHAURI NA KATA YA MIKUMI WAKIJADILIANA JAMBO FULANI KUHUSU UJENZI WA MADARASA SHULE YA SEKONDARI MIKUMI HUKU UJENZI UKIENDELEA.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa