Ruaha ni miongoni mwa kata arobaini zilizopo wilayani Kilosa ambapo wananchi wa kata hiyo wamelazimika kutimiza wajibu wao wa kikatiba kwa kupiga kura siku ya tarehe 28 November,2024 kutokana na mivutano iliyosababishwa na baadhi ya wananchi wachache kugoma na kukwamisha zoezi hilo.
Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Ndg. Michael J. Gwimile amesema kuwa zoezi la upigaji kura kwa Kata ya Ruaha limelazimika kuharishwa siku ya tarehe 27 kutokana na changamoto zilizojitokeza ambazo zingepelekea hali ya uvunjifu wa Amani hivyo ikalazimika uchaguzi huo kufanyika tarehe Novemba 28, 2024.
“Tuliona ni busara kuhahirisha kwanza ili kila mtu ashuke chini pawe na utulivu na tuimarishe hali ya ulinzi na usalama kwa watu wote wenye nia njema na wanaotaka kushiriki uchaguzi hilo ndo jambo ambalo viongozi tulilifanya ” Alisema Gwimile.
Wakati wananchi wakiendelea na uchaguzi huo, baadhi yao walieleza hali ya kidemokrasia imechangia kuongezeka kwa hamasa kubwa kwa wananchi kujitokeza kuchagua viongozi wanaoamini kuwaletea maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa