Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaji Majid Hemed Mwanga ametoa rai kwa Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini(RUWASA) na Mamlaka ya Maji Morogoro(MORUWASA) kufanya kazi kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali ili kuibua vyanzo mbalimbali vya maji wilayani Kilosa.
Rai hiyo imetolewa Agost 2,2022 wakati akikabidhi pikipiki na tanki za maji kwa watumia maji ambapo amesema kuwa iwapo watashirikiana na taasisi nyingine kubuni vyanzo vipya vya maji wananchi watapata maji ya kutosha kwani bado kuna changamoto za upatikanaji wa maji kwa baadhi ya maeneo.
Mwanga amesema Serikali bado inaendelea na jitihada za kuboresha huduma ya maji vijijini na mijini na kiwango cha upatikanaji wa maji kinakua siku hadi siku ambapo hali ya upatikanaji wa maji kwa Kilosa umekua kutoka asilimia 67.75 mwaka 2018 na kufukia asilimia 73.00 mwaka 2021 ukuaji ambao umechangiwa kwa kiasi kikubwa na uwekezaji unaofanywa na Serikali na wadau wa Maendeleo kutokana na Serikali kuwa na mahusiano mazuri na wadau hao.
Aidha amesisistiza kuendela kujenga mahusiano mazuri na viongozi wa wa Serikali za Vijiji na Kata kwani ndio wanaokaa na wananchi katika maeneo wanayofanyia kazi huku akitaka kufikia Disemba 30 2022 kila chombo kiwe kimeandaa mpango wake wa biashara wa miaka mitatu na ifikapo Mei 2023 vyombo vyote viwe vimeandaa na kuwasilisha maombi ya bei mpya.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa