Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Mashariki Morogoro imetembelea na kufanya kikao na watumishi wa Makao Makuu Halmshauri ya Kilosa kwa lengo la kuwakumbusha na kuwaelimisha watumishi kuenenda na kanuni mbalimbali za kiutumishi ili ziwasaidie katika utendaji kazi.
Wakati wa kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Wilayani hapo Mei 9, 2024 Afisa Maadili Bw. Yahya Tumba kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Mashariki Morogoro ameeleza na kufafanua kanuni na maadili za utendaji kazi.
Kanuni hizo ni pamoja na; Kuheshimu haki za binadamu/ mtumishi wa umma, Nidhamu, juhudi na bidii katika utekelezaji wa majukumu, Kufanya kazi kwa ushirikiano, Kutoa huduma bora, Kufanya kazi kwa kuambatana na Tabia njema/nzuri, Uwazi na uwajibikaji, Kufanya kazi kwa uadilifu pamoja na Kutojihusisha na masuala ya kisiasa kwenye maeneo ya kazi.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa