Uwanja wa ndege wenye urefu wa Kilometa 5.4 kujengwa ndani ya wilaya ya Kilosa ili kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji ikiwa ni pamoja kufungamanisha miundombinu ya usafirishaji kwa njia ya Reli ya Kisasa, barabara na njia ya anga.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka wakati akihutubia katika kikao maalumu cha kamati ya ushauri ya wilaya (DCC) uliofanyika 25 Februari, 2025 katika ukumbi wa MT.
Mhe. Shaka amesema kuwa uwanja huo ambao ulisitisha kutoa huduma kwa takribani miaka 20 iliyopita, ukikamilika utakuwa na uwezo wa kupokea ndege kubwa na ndogo huku akifafanua kuwa kukamilika kwa uwanja huo kutarahisisha shughuli za utalii na usafirishaji wa abiria na mizigo.
Katika hatua nyingine, Mhe. Shaka amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne, serikali imetekeleza miradi mingi ya maendeleo ndani ya wilaya katika sekta za afya, maji, elimu na miundombinu ya barabara huku akiishukuru serikali kwa kutoa fedha nyingi za miradi hiyo.
Aidha, amewataka watendaji wa serikali, wanasiasa wakiwemo madiwani na wananchi kwa ujumla kushiriki zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga kura linalotarajia kuanza tarehe 01 hadi 07 Machi, 2025 katika majimbo ya Kilosa na Mikumi.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa