Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Greyson Msigwa amesema kuwa serikali imekamilisha ujenzi wa Mradi wa Julius Nyerere Hydropower Project (JNHPP) kwa asilimia 99.8 wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2115 utakaosaidia kusambaza umeme nchini.
Msigwa ametoa taarifa hiyo 16 Februari 2025 alipokuwa katika Mkutano na waandishi wa habari katika eneo la Mradi wa Julius Nyerere Rufiji Mkoani Pwani uliokuwa na lengo la kutoa taarifa ya kile kinachoendelea katika Mradi huo wa Kuzalisha Nishati ya Umeme.
Msigwa ameongeza kuwa mradi huo umesaidia kupunguza changamoto ya kukatika kwa umeme hapa nchini na kwasasa kama changamoto hiyo ipo basi ni kutokana na Miundombinu chakavu iliyopo ambayo nayo itafanyiwa marekebisho ili kuondoa kabisa adha hiyo kwa baadhi ya maeneo.
Aidha Msigwa amesema kuwa Watanzania Wachangamkie fursa zilizopo katika mradi huo ambao utahusisha mambo matatu ikiwemo Upatikanaji wa umeme wa uhakika, kilimo cha umwagiliaji na shughuli za uvuvi.
Mradi wa Mwalimu Julius Nyerere umegharimu kiasi cha shilingi Tirioni 6.558 fedha kutoka serikali kuu ambapo mpaka sasa mradi huo upo hatua ya umaliziaji kukamilika sambamba na hayo Msigwa ametoa wito kwa Watanzania kuitunza miradi hiyo na kuacha kufanya uharibifu kwa makusudi.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa