Katika kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali zinafanya kazi stahiki kulingana na thamani ya fedha Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Comrade Shaka H. Shaka ameendelea na ziara yake ya kikazi katika kukagua miradi ya maendeleo katika tarafa ya Magole katika ya kata ya Dumila na kuonyesha kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Shaka akiwa katika ziara hiyo akiwa ameongozana na Kamati ya Ulinzi na usalama Wilaya pamoja na wataalam wa Halmashauri ameitumia vema kwa kusikiliza kero za wananchi kwa lengo la kupata suluhu pamoja na kusikiliza ushauri mbalimbali toka kwa wananchi ili kuiletea maendeleo Wilaya ya Kilosa.
Akiwa katika mkutano wa hadhara Shaka amewaahidi wananchi kuwashirikisha katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo changamoto ya migogoro ya wakulima na wafugaji ambapo amesema Wilaya imeandaa mkakati wa utatuzi wa changamoto hiyo ambao unatarajiwa kushirikisha wananchi ili kuhakikisha changamoto hiyo inatatuliwa katika njia shirikishi
Aidha katika ukaguzi huo licha ya kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo kwa kiasi kikubwa ametoa kasoro zilizojitokeza katika miradi miwili ambayo ni majengo ya kituo cha Afya Dumila mradi wenye thamani ya shilin gi milioni 500 pamoja na jengo la shule ya mpya ya sekondari Dumila wenye thamani ya shilingi milioni 125 ambapo ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kuipitia kwa upya miradi hiyo ili kubaini ubora na thamani ya fedha zilizotumika katika miradi hiyo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa