Kati ya mwaka 2019 na 2021 watu 26 wamepoteza maisha wakati wakivuka katika mto Ruhembe kwa kusombwa na maji katika kipindi cha mvua za masika kutokana na eneo hilo kukosekana kwa darajamkatika eneo hilo ambapo kufuatia tukio hilo Serikali imepeleka zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 40 la mto Ruhembe hivyo kukamilika kwake utakua mwarobaini wa changamoto hiyo.
Akizungumza katika hafla ya mkandarasi Fomast Campany limited kukabidhiwa eneo la mradi wa ujenzi wa daraja hilo Diwani wa kata ya Ruhembe, Salum Mponzi amesema kumalizika kwa ujenzi wa daraja hilo itakuwa faraja kwa wakazi wa kata nne za Kidodi, Ruhembe, Ruaha na Vidunda kutokana na jamii za wananchi hao kutegemeana katika mahitaji mbalimbali.
Mponzi amesema ana amini daraja hilo litakuwa mkombozi kwa wananchi wa kata hizo ambazo wanategemeana zaidi katika shughuli za kilimo na mahitaji mbalimbali huku akisema kuwa kazi iliyopo mbele yao ni kushirikiana na mkandarasi katika kutunza vifaa pindi vitakapoletwa na kuwa wananchi wa maeneo hayo watafaidika na mradi huo Wakati wananchi wakiweka matumaini ya daraja hilo ili kuwaondoa adha wanazopata,
Wakati wananchi wakiweka matumaini ya daraja hilo ili kuwaondoa katika adha wanazopata, Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Alhaji Majid Mwanga ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa mkandarasi lakini huku akiwaonya wazazi ambao hawajawaapeleka shule watoto kwa visingizio mbalimbali kuchukua hatua za dhati na kuwapeleka shule watoto hao ili wapate haki ya elimu huku Mbunge wa jimbo la Mikumi Mh. Dennis Londo akisema Serikali sikivu ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kusikia kilio cha wakazi wa Ruhembe inatenga zaidi ya shilingi bilioni moja na kumkabidhi mkandarasi ili kufikia mwezi June 2022 wananchi wa kata hiyo wawe wanapita juu ya daraja na hivyo kunusuru maisha yao
Naye Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini Wilaya ya Kilosa (Tarura), Mhandisi Harold Sawaki amesema mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.1 na daraja hilo litakuwa na urefu wa mita 40 huku likitarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi mitano kuanzia muda waliosainiana na mkandarasi huku Meneja wa kampuni ya Fomast Campany limited Dar es Salaam, Hanaf Mbaruku akitaka wananchi na viongozi kutoa ushirikiano mkubwa wakati wote wa mradi huo lakini kujiepusha na matukio ya wizi wa vifaa kwani itakuwa kukwamisha kazi isimalizike kwa wakati.
Kwa niaba ya wakazi wa kijiji cha Ruhembe, Mwalimu Rose Mremba amesema kuwa nyakati za masika wamekuwa wakitumia fedha nyingi kati ya sh5,000 hadi sh10,000 kufika upande wa pili kama gharama za usafiri ambapo maji yakiwa kidogo kiasi mtoni utavushwa kwa sh5,000 kwa kubebwa mgongoni lakini yakijaa utaweza kukodi usafiri hadi sh10,000.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa