Katibu Tawala Wilaya Yohana Kasitila ametoa wito kwa wakuu wa shule mbalimbali zilizoweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mitihani ya kidato cha nne 2019 kushirikisha viongozi wa serikali za vijiji sambamba na jamii inayowazunguka katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika uendeshaji wa kambi hizo hususani suala la uchangiaji wa chakula kwa ajili ya watoto hao.
Kasitila amesema hayo Agosti 19/08/2019 wakati alipotembelea shule za sekondari zilizopo tarafa ya Mikumi na Ulaya ikiwemo kambi ya Masanze inayojumuisha shule za Mati Tindiga, Masanze, Zombo na Kilangali huku shule nyingine zilizotembelewa ni Mikumi, Iwemba na Kidodi ambapo miongoni mwa changamoto zilizobainishwa ni upungufu wa chakula ambacho kinachangiwa na wazazi wa watoto husika
Kasitila amesema kuwa viongozi wa serikali za vijiji wakishirikishwa kikamilifu hamasa ya uchangiaji itakuwa kubwa ikiwemo kupata michango toka katika misikiti na makanisa kupitia viongozi wa dini sambamba na kuwashirikiasha wafanyabiashara na taasisi mbalimbali.
Aidha amezitaka shule ambazo bado hazijaanza kambi kuanza kambi hizo mara moja ambapo agizo lilitolewa na Mkuu wa Wilaya kuanza kambi hizo tarehe 01/8/2019 lengo ikiwa ni kufikia malengo ya wilaya kufuta daraja ziro na daraja la nne ambapo kupitia kambi hizo zitakazokuwa zikifundishwa na walimu mahiri zitaleta matokeo chanya na kuongeza kiwango cha ufaulu .
Pamoja na hayo ameendelea kuwakumbusha walimu katika kambi zote kuhakikisha wanaweka utaratibu wa kujipima kile wanachowekeza kwa wanafunzi kwa kutoa majaribio na mitihani ili kuona uelewa wa wanafunzi hao sambamba na kuona matokeo ya uwepo wa kambi hizo.
Pamoja na hayo ametoa kwa wanafunzi wa kidato cha nne kutumia vema fursa za uwepo wa kambi hizo kusoma kwa bidiii ili kupata matokeo tarajiwa ya ufaulupamoja na kufuta daraja ziro na la nne ambayo yatawasaidia kuendelea na kidato cha tano sambamba na kuwa na maisha mazuri hapo baadae
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa